Loading...
title : CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua.
link : CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua.
CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua.
Na. IS-HAKA OMAR, Zanzibar..
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kinaendekea na juhudi za kuishauri serikali iharakishe utaratibu wa kutoa misaada kwa wananchi walioathiriwa na maafa ya mvua ili waweze kupata huduma za msingi kama walivyo wananchi wengine waliosalimika na tatizo hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Dkt.Abdalla Juma Saadala '' Mabodi" katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maeneo mbali mbali nchini yaliyopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Dkt.Mabodi aliwambia wananchi hao kwamba serikali ya Mapinduzi ya zanzibar inayotokana na chama hicho ni sikivu na inathamini maisha na utu wa wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa, hivyo itaendelea kutoa mapendekezo kwa Idara ya Maafa nchini ifike kila pembe ya visiwa vya zanzibar kuhakikisha wananchi wote waliopata maafa wanaratibiwa na kupatiwa misaada.
Alieleza kwamba pamoja na taasisi hiyo kufanya kazi za kisiasa bado ina jukumu la kuwalinda na kuwasaidia wananchi wakati panapotokea majanga mbali mbali ya kitaifa ili waweze kubaki salama na kuendelea na shughuli za kimaendeo.
"Wananchi tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atuvushe salama katika hii neema ya mvua iliyochanganyika na mitihani, ili turudi katika maisha ya kawaida na kuondokana na hofu.
Jukumu letu kama chama cha kisiasa wakati wa maafa ni kuhakikisha kila mwananchi ana kuwa salama na kupata huduma za msingi sambamba na kuwafariji huku serikali ikiendelea kukamilisha taratibu za kutafuta ufumbuzi wa kumaliza changamoto zinazotokana na maafa hayo." alieleza Dkt. Mabodi wakati akitoa msaada wa fedha sh.200,000 kwa mwananchi wa Shehia ya Miwani Unguja, Bw.Endward Maziku ambaye nyumba yake imebomoa na kukosa makaazi ya kuishi.
Akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa maeneo ya shehia ya Miwani kuwa changamoto ya miundo mbinu ya barabara inayowakabili , alisema SMZ ina mpango wa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu pamoja na Vijiji vya Koani, Jendele, Unguja Ukuu na Jumbi.
Alifafanua kuwa baadhi ya barabara hizo tayari zilikuwa zimeanza kutengenezwa lakini baadae serikali ikabaini kuwa Mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hana sifa na ikaamua kumfuta.
Sambamba na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo, aliendelea kuwasisitiza waakazi wa maeneo mbali mbali kutibu maji kabla ya kuyatumia pamoja na kuwa karibu na watoto wadogo wasicheze karibu na mabwawa ya maji ya mvua kwa lengo la kuepuka athari za maafa.
" Nakiri kwamba mvua hizi ni kubwa sana hazijawahi kutokea kwa miaka ya hivi karibu, kwani mvua kama hizi nakumbuka zilitokea miaka ya 1972-1973 na kuacha maafa makubwa.
Pia nawaomba wanasiasa nchini tusitumie maafa haya kama ajenda ya kisiasa bali tuwafariji na kutoa nasaha za kuwashauri mambo mema na kuwaeleza hali halisi kwani SMZ na CCM hazipendi wananchi wapate majanga na migogoro, hivyo mitihani hiyo ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu".alifafanua Naibu Katibu Mkuu huyo.
Mapema wananchi hao kwa nyakati tofauti walisifu kasi ya usimamizi wa Ilani ya CCM inayotekelezwa na Serikali kwa kuimarisha huduma za msingi katika sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi.
Akizungumza Mkaazi wa Chwaka Wilaya ya Kati alisema licha ya kuwepo kwa changamoto za maafa zilizoharibu miundombinu ya maji, barabara na umeme lakini bado wana matumaini kwa serikali itafanya marekebisho ya haraka kwa baadhi ya huduma ili zilidi katika hali ya kawaida.
Naye Mkaazi wa Jambiani Kikadini, Ramadhan Kassim, aliwaomba wananchi wa maeneo mbali mbali nchini kuwa na utamaduni wa kuwa na tahadhari ya kujipanga mapema kwa kufuata ujenzi unaozingatia ushauri wa kitaalamu ili kuepuka maafa wakati wa mvua zijazo.
Hivyo makala CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua.
yaani makala yote CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/ccm-zanzibar-yaahidi-kuishauri-smz.html
0 Response to "CCM Zanzibar Yaahidi Kuishauri SMZ Iharakishe Misaada Kwa Waathirika wa Mvua."
Post a Comment