Loading...
title : Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo
link : Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo
Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mtafiti wa masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Haji Semboja anasema kuwa amefurahishwa na ripoti ya Kamati Maalum iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ya kuchunguza mchanga wa madini kwenye makontena 277 yaliyozuiwa na serikali kusafirishwa kwenda nje kwaajili ya uchenjuaji.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mahojiano na mwandishi wa habari hii, Dkt.Semboja alisema kuwa, hatua hiyo ni nzuri na ya kuridhisha kwa vile Rais Magufuli amefanyia kazi suala hilo ambalo limekua likizungumzwa kwa muda mrefu na baadhi ya wasomi,wanaharakati na hata wanasiasa hapa nchini.
“Mimi ni kati ya Watanzania waliofurahishwa na maamuzi ya Rais, nina furaha kubwa hasa ukizingatia niliwahi kushiriki katika uandaaji wa sera za madini na uwekezaji, na ni wazi kuwa tumekuwa tukiibiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta ya madini” alisema Dkt.Semboja.
Malalamiko haya ya wizi na utoroshaji wa madini yamekuwepo kwa muda mrefu, kitu ambacho tulikua tukizungumza sasa kimethibitishwa , baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti hiyo ya mchanga”, aliongeza Dkt.Semboja.
Aidha, Dkt.Semboja amemshauri Rais Magufuli kuendelea kuwatumia wataalamu mbalimbali waliopo nchini na kuiomba Serikali iwe na utaratibu wa kuwatumia watu wake ambao wengi ni wazalendo na wana uchungu na nchi yao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo
yaani makala yote Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/dktsemboja-amsifu-rais-magufuli-kuhusu.html
0 Response to "Dkt.Semboja amsifu Rais Magufuli kuhusu ripoti ya mchanga, Awataka watanzania kumsaidia katika vita hiyo"
Post a Comment