Loading...
title : HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG
link : HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG
HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG
Na: Elinipa Lupembe
Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha wamekubaliana kutoa ushirikiano mkubwa kwa wataalamu wa halamashauri ya Arusha katika kusimamia Miradi kupitia Mfumo Mpya wa Ruzuku ya Serikali ya Miradi ya Maendeleo Local Government Development Grant ' (LGDG ).
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Mh. Noah Lembri wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya Mafunzo ya siku moja ya Mfumo Mpya wa ruzuku ya serikali ya Miradi ya Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Halamashauri ya Arusha.Mh. Lembris amesisitiza kuwa wajumbe wa baraza la madiwani liko tayari kushirikiana na watumishi wote kusimamia fedha za ruzuku za miradi ya maendeleo kwa kuwa lengo la mfumo ni kuhakikisha miradi inasimamiwa vizuri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.Mwenyekiti Lembris amewataka wataalamu wote kusimamia fedha za miradi kwa kufanyakazi kwa nidhamu, uadilifu kwa kufuata miongozo, kanuni, sheria na taratibu za matumizi ya fedha za serikali.Pia ameutaka uongozi wa halmashauri kuwa wawazi na kutoa taarifa mapema endapo kuna tatizo lolote kuliko kukaa kimya mpaka mambo yaharibike 'Watendaji wanatakiwa kuwa wazi kwetu na kama kuna tatizo tushirikisheni mapema ili tutoe ushauri kabla mambo hayajaharibika' alisema Mh. Lembris Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha ameahidi kusimamia vema mfumo huo na kuwashughulikia watumishi watakaoenda kinyume na taratibu hizo.'Nitakua serious na usimamizi wa miradi na mtumishi atakayeleta uzembe nitamshughulikia' alisisitiza Dkt.MaheraMkutano huo licha ya kujifunza mfumo wa mpya wa ruzuku ya serikali pia mkurugenzi wa halmashauri aliwasilisha taarifa ya Mpango Mkakati wa halamashauri ya Arusha kwa miaka mitano ambao madiwa hao waliupitisha na kuomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa watendaji wa halmashauri sambamba na kubuni miradi ya kuongeza mapato ndani ya halmashauri.Pichani ni matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Hivyo makala HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG
yaani makala yote HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/halmashauri-ya-arusha-yapitisha-mfumo.html
0 Response to "HALMASHAURI YA ARUSHA YAPITISHA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MIRADI LGDG"
Post a Comment