Loading...
title : ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI
link : ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI
ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI
Na John Luhende
mwambawahabari
Kampuni ya simu za mikononi ya Itel Leo imemtambulisha rasmi Msanii maarufu wa bongo muvi nchini Irene Uwoya kuwa balozi mpya wa Itel Mobile Tanzania kwa kipindi cha mwaka moja kuanzia sasa.
Akimtambulisha balozi huyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Asha Mzimbili , Amesema wamemchagua Irene Uwoya kwa kutambua mchango wake Mkubwa kwenye jamii kwa kuelimisha wananchi kupitia filamu zake.
Aidha ameongeza kuwa wanatarajia jamii itafaidika kwa kupata Elimu kuhusu bidhaa zao kupitia kwa balozi huyo .
"hivyo tutashirikiana nae hasa kwenye matukio mbalimbali yaliyopo ndani ya jamii kwa kutoa michango na Msaada kwa makundi ambayo tunayaendesha."
Afisa huyo akaongeza kwa kusema kuwa kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano pamoja na vifaa vyake Itel Mobile imeendelea kutengeneza simu bora ambazo zinaendana na mahitaji ya wateja wao.
"Tunazalisha bidhaa bora kwa sababu tunaamini kwamba tunapoipatia jamii bidhaa za mawasiliano zenye ubora na viwango vya juu,kuridhisha tunaifanya jamii kuungana na jamii nyingine za kimataifa kushirikiana katika kuleta Maendeleo na maisha bora zaidi."
Kwa upande wake balozi huyo mpya amemshukuru kampuni hiyo kwa kutambua mchango wake na kusema kuwa atajitahidi kuwa balozi mzuri kwa kutangaza simu za kampuni hiyo na kwa kuanzia amewataka wananchi kuchangamkia simunmpya za kampuni hiyo aina ya Itel S 31 ambazo tayari zipp sokoni kote nchini.
Hivyo makala ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI
yaani makala yote ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/itel-yamtambulisha-iren-uwoya-kuwa.html
0 Response to "ITEL YAMTAMBULISHA IREN UWOYA KUWA BALOZI WAKE MPYA NCHINI"
Post a Comment