Loading...

ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI

Loading...
ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI
link : ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI

soma pia


ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wananchi kutumia fursa ya huduma za msaada wa kisheria ambayo inatolewa nchini ili kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati.

Amesema wananchi wakiitumia huduma ya msaada wa kisheria itawawezesha kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati , kufahamu sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu unaotumiwa na Mahakama na hivyo kusaidia harakati za kupunguza msongamano Mahakamani.

 “Wananchi niwaombe mtumie fursa ya msaada wa kisheria ambayo Serikali imeridhia itolewe kwa wananchi wenye uhitaji, hii itasaidia kutambua haki zenu, kufahamu sheria na utaratibu unaotumika na Mahakama na hivyo kusaidia kupunguza msongamano Mahakamani” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi amesema hayo mjini Morogoro alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini ambayo inafanyika katika mikoa ya Morogoro, Singida, Tabora, Kagera na Kigoma kuanzia tarehe 26 Novemba hadi tarehe 30 Novemba ,2018. 

Amesema Wizara itaendela kutenga wiki moja kila mwaka kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria nchini ili kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na huduma za msaada wa kisheia na hivyo kutimiza lengo la kutungwa kwa Sheria Na. 1 ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimpa mkono msanii Afande Sele baada ya kumaliza kutumbuza katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro 
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiangalia kitabu katika moja ya mabanda yaliyohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro , Prof. Kabudi alitembelea mabanda hayo baada ya kuzidua maadhimisho hayo mjini Morogoro 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza katika banda la Mahakama ambalo linashiriki maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria nchini ambayo ufunguzi wake kitaifa ulifanyika mkoani Morogoro uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro 
Wananchi waliofika kupata huduma ya msaada wa kisheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa wiki hiyo mjini Morogoro. 
Wanasheria wa kujitegemea mkoani Morogoro katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa maadhimisho y awiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro . 




Hivyo makala ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI

yaani makala yote ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/itumieni-fursa-ya-msaada-wa-kisheria.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI"

Post a Comment

Loading...