Loading...

Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge

Loading...
Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge
link : Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge

soma pia


Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge


Joyce Kasiki, Dodoma

Jenista Mhagama
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, amesema hajajua bajeti ya ukimbizaji Mwenge wa Uhuru kwa nchi nzima kutokana na gharama hizo kutofautiana kwa halmashauri.

Mhagama alitoa kauli hiyo jana akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy aliyetaka kujua ni kiasi cha fedha zinazotumika kukimbiza Mwenge nchi nzima kwa mwaka.

Waziri huyo alisema bajeti ya Mwenge huandaliwa na halmashauri husika kwa lengo la kufanikisha mbio hizo.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji alitaka kujua kama Mwenge kusudio lake ni umoja, upendo na mshikamano ni sababu gani umegeuka kueneza chuki kwa kuadabisha au kuwaweka mahabusu baadhi ya wenyeviti wa mitaa kutokana na kushindwa kuchangisha fedha za mbio hizo.
  
Pia alitaka kujua kama kuna faida kwa Watanzania kuendelea kukimbiza Mwenge huo kila mwaka na kama kuna faida ni zipi.

Akijibu swali hilo, Mhagama alisema faida za Mwenge kitaifa na kimataifa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali.

Aidha, alisema Mwenge ni chombo pekee cha kujenga umoja na mshikamano na kudumisha amani pale unakopita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa.

“Mfano mzuri ni kutokana na takwimu ambazo zinaonesha kuwa miradi ya maendeleo iliyozinduliwa pamoja na kuwekwa mawe ya msingi kupitia Mwenge wa Uhuru kwa mwaka juzi ni 1,342 yenye thamani ya Sh bilioni 463.5,” alisema Mhagama.

Alisema Serikali haina mpango wa kusitisha mbio hizo kutokana na faida na mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia mbio hizo.


Hivyo makala Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge

yaani makala yote Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/jenista-sijui-bajeti-ya-mwenge.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jenista: Sijui bajeti ya Mwenge"

Post a Comment

Loading...