Loading...

NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA

Loading...
NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA
link : NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA

soma pia


NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA

Mwambawahabari

NHC-1
Na Jacquiline Mrisho 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeishauri Serikali kuifanya bima ya afya iwe lazima kwa kila mwananchi na sio hiari kama ilivyo sasa.
Ushauri huo umetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Benard Konga alipokuwa akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

“Ifike wakati suala la bima liwe ni lazima sio hiari na kwamba lengo sio kukusanya fedha nyingi bali kumpunguzia mwananchi gharama za matibabu na kuhakikisha mwananchi huyo anapata huduma bora za afya kwa wakati wote anapohitaji matibabu”alisema Konga.
Konga alieleza kuwa mpango wa baadae wa Mfuko huo ni kuongeza hamasa itakayopelekea wananchi wengi zaidi kujiunga na bima za afya ili  kutimiza lengo la kufikia asilimia 75 ya wananchi wote kuwa na bima ya afya ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 29 iliyopo hivi sasa.
Kaimu Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa mfuko huo hivi sasa unahudumia zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanaoishi vijijini.
Kwa upande wa utoaji huduma, Konga alieleza kuwa Mfuko huo umesajili jumla ya vituo 6600 vinavyotoa huduma kwa bima ya afya pamoja na maduka ya madawa 200 yanayotoa dawa kwa kutumia bima ya Mfuko huo.
Hata hivyo, alitoa rai kwa hospitali mbalimbali nchini kuzingatia  masharti na vigezo vilivyowekwa katika utoaji wa huduma za bima na kuepuka tabia ya kunyanyasa wanachama wa Mfuko huo.
Aidha, amewataka waajiri kuiga mfano wa Serikali katika suala zima la kupeleka kwa wakati michango ya wanachama.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzishwa mnamo mwaka 1999 baada ya Serikali kupitisha Sheria ya kuruhusu Mfuko huo ambapo mwaka 2001 ulianza rasmi kutoa huduma kwa watumishi wa umma. Mwaka huo huo,marekebisho ya sheria yalifanyika kuruhusu Mfuko huo kutoa huduma kwa wananchi walio katika sekta zisizo rasmi.


Hivyo makala NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA

yaani makala yote NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/nhif-waishauri-serikali-bima-ya-afya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA"

Post a Comment

Loading...