Loading...
title : NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA
link : NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA
NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA
Akiongea na wanahabari ofisini kwake, Almas amesema,NRA wamepokea kwa mstuko taarifa hiyo ya ajali na vifo vya wanafunzi ambao ni nguvu kazi ijayo ya Taifa letu.
Kwa niaba ya NRA, Almas amewataka wazazi ,Ndugu ,jamaa ,wana Arusha na watanzania kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Pmoja na salama hizo za pole, Almas amewataka madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali zinazochangia vifo vingi vinavyopoteza hazina ya Taifa.
"Vijana hawa ndio hazina ya taifa hili, na ndio akiba ya ujuzi na utaalamu wa taifa,ajali hii imepoteza wabunge,mawaziri, walimu, madaktari ,wachumi,wanasiasa,askari ,marubani na hata wanasayansi wa miaka ijayo,huu ni msiba mkubwa kwa Taifa letu",amesema Almas.
Katibu Mkuu huyo ameliomba jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali na amewashauri wanahabari kuandaa makala maalum katika vyombo vyao vya habari juu ya suala zima la usalama sio makala za siasa pekee.
Alisema"nyie wana Habari ni wadau wakubwa sana wa usalama barabarani maana nanyi ama jamaa zenu ni wasafiri, madereva,mnapotumia muda mwingi kuandika makala za siasa pia muandike Makala za usalama barabarani ili kulisaidia jeshi la polisi ktk kazi hii ya kutoa elimu"
Almas pia amemtaka mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani kukutana na wanasiasa ili kubadilishana mawazo juu ya kushirikiana nao katika kutoa elimu hiyo kwa wanachama wetu katika mikutano yao ya kisiasa inayohudhuriwa na watanzania wengi.
"Natoa ushauri kwa Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mohamed Mpinga kukutana na viongozi wa juu wa vyama vya siasa ili kubadilishana uzoefu,kutoa mafunzo mafupi na kutupatia vipeperushi vya elimu ya usalama barabarani ili tuwapatie wanachama wetu katika mikutano yetu ya kisiasa" ,alisema Almas.
Alijikita zaidi na kutoa mfano wakati wa uongozi wa IGP mstaafu Said Mwema, suala la utii wa sheria bila shuruti wanasiasa walikuwa wakikutana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya usalama na hatimaye kuwapatia vipeperushi vya elimu hiyo utii wa sheria nao waliweza kuwapa elimu hiyo wanachama wao., hili sio jambo la jeshi pekee maana jeshi lina kazi nyingi na muhimu ,nao kama wanasiasa wanao wajibu wa kusaidia jeshi letu.
KATIBU MKUU wa chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Hassan Kisabya Almas akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani na kuwapa pole watanzania kwa msiba uliotokea jana wa vifo vya wanafunzi vilivyotokea Mkoani Arusha.
Hivyo makala NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA
yaani makala yote NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/nra-yatoa-pole-kwa-wafiwa-na-wakazi-wa.html
0 Response to "NRA YATOA POLE KWA WAFIWA NA WAKAZI WA ARUSHA KWA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA"
Post a Comment