Loading...
title : “SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA
link : “SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA
“SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA
MwambawahabariSerikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa inategemea kusambaza vifuko maalum vya kujifungulia vyenye vifaa vya kujifungulia kwa wanawake 500,000 ambavyo vitasambazwa nchi nzima kulingana na uhitaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhe.Dk Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatibu leo Bungeni Mjini Dodoma.
“Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaeleza kuwa Huduma za kina Mama wajawazito katika vituo vya ngazi zote zinapaswa kutolewa bila malipo”,Alisisitiza Mhe.Kigwangala
Aidha amesema kuwa Serikali haijawahi kuweka tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji na hivyo huduma hizo zitaendelea kutolewa katika ngazi zote katika vituo vya umma vya kutolea huduma kwa gharama za Serikali.
Aidha kwa upande mwingine Mhe,Kigwangala ametoa rai kwa Wabunge kusaidia kusimamia utekelezaji wa Sera walizokubaliana katika katika maeneo yao husika ili kuhakikisha huduma hizi za kina mama zinapatikana kwa Gharama za Serikali kama ilivyopangwa.
“Ili azma ya Serikali ya Kuhakikisha akina mama wajawazito wanapata huduma nzuri na lengo la kupunguza vifo vya mama na watoto inafanikiwa ni lazima usimamizi uwe wa karibu sana”,Aliongeza Mhe.Kigwangalla.
Aidha jumla ya kina mama 1,900,000 hujifungua kila mwaka nchini na kumekuwa na changamoto katika upatikanaji wa vifaa ambapo kwa sasa Serikali imeliwekea mkazo suala hilo ili kuhakikisha kina mama hao wanajifungua salama.
Hivyo makala “SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA
yaani makala yote “SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala “SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/serikali-kusambaza-vifuko-vyenye-vifaa.html
0 Response to "“SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA"
Post a Comment