Loading...
title : Serikali yafikiria wazee wa mabaraza
link : Serikali yafikiria wazee wa mabaraza
Serikali yafikiria wazee wa mabaraza
Joyce Kasiki, Dodoma
SERIKALI inaangalia uwezekano wa kuongeza posho ya wazee wa mabaraza ya Mahakama nchi nzima kutokana na kiwango cha sasa Sh 5,000 kuwa kidogo, pia kupunguza vitendo vya rushwa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbagala, Ali Mangungu (CCM).
Katika swali lake, Mangungu alitaka kujua kama Serikali haioni kuwa inachochea rushwa kwa kutoa kiasi hicho kidogo cha posho kwa wazee hao.
Awali katika swali la msingi, Mbunge huyo alitaka kujua kama Serikali haioni ni wakati mwafaka sasa kuwaongeza posho wazee hao hususan wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, ambao wamekuwa wakisikiliza kesi nyingi zikiwamo za mauaji.
Akijibu swali hilo, Profesa Kabudi alisema Serikali itawaongeza posho wazee hao kwa kadri bajeti itakavyopatikana.
Aidha alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee wa Baraza katika Mahakama nchini na umuhimu wa kutoa posho kama motisha na kwamba kutokana na umuhimu huo, ingetamani posho za wazee hao ziongezeke ili kuendana na hali ya maisha.
Alisema kwa bahati mbaya posho hizo hutokana na bajeti ya matumizi mengineyo ambazo hutengwa na Serikali kwa kila fungu.
Hata hivyo Profesa Kabudi alisema kwa mwaka wa fedha 2016/17, Mahakama ya Tanzania ilitengewa Sh bilioni 1.27 na mwaka 2017/18 Mahakama imetengewa Sh bilioni 1.85 kwa ajili ya malipo ya posho ya wazee wa mabaraza.
Alisema Serikali itaendelea kutenga au kuongeza posho kwa malipo mbalimbali zikiwamo posho kwa ajili ya wazee hao.
Hivyo makala Serikali yafikiria wazee wa mabaraza
yaani makala yote Serikali yafikiria wazee wa mabaraza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yafikiria wazee wa mabaraza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/serikali-yafikiria-wazee-wa-mabaraza.html
0 Response to "Serikali yafikiria wazee wa mabaraza"
Post a Comment