Loading...
title : Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa.
link : Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa.
Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa.
Na Pascal Mayalla
Taasisi ya TradeMark East Africa inazijengea uwezo bidhaa za Tanzania ili kuziingiza kwenye masoko ya kimataifa, kwa kuziwezesha kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa.
Kwa hatua hiyo bidhaa hizo zitakuwa na uwezo wa kuhimili ushindani wa kimataifa na kuingia kwenye masoko ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bara la Afrika na masoko ya kimataifa yakiwemo masoko ya Ulaya na Marekani, amesema Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga kwenye kongamano ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam Jumamosi.
Bw. Ulanga amesema zoezi la kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinafikia viwango vya ubora wa kimataifa, linafanywa kwa kupitia mafunzo ya viwango vya ubora kwa kuzitumia taasisi za TBC, TFDA na GS 1 kwa ajili ya barcode kwa bidhaa za Tanzania, hivyo bidhaa hizo kuweza kuhimili ushindani katika masoko ya kimataifa kwa kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa.
Bw. Ulanga amesema mafunzo hayo yanaendeshwa kwa awamu mbalimbali, ni sehemu ya utakelezaji wa mradi mkubwa wa Taasisi ya Trademark East Africa ujulikanao kama “Women in Trade” unaolenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa ambapo Taasisi ya TradeMark imetenga Dola za Marekani zaidi ya Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania kugharimia mpango huo.
Mwenyekiti wa TWCC, Mama Jaquline Maleko akizungumza.
|
Washirika wa mafunzo hayo,
Washirika wa mafunzo hayo,
Washirika wa mafunzo hayo,
Hivyo makala Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa.
yaani makala yote Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/taasisi-ya-trademark-east-africa-tmea.html
0 Response to "Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) yazijengea Uwezo bidhaa za Tanzania kuingia masoko ya kimataifa."
Post a Comment