Loading...

VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18

Loading...
VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18
link : VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18

soma pia


VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na  vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali  utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/05/2017



Hivyo makala VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18

yaani makala yote VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/vyuo-binafsi-sasa-kudahili-wenyewe.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VYUO BINAFSI SASA KUDAHILI WENYEWE WANAFUNZI WA CHETI NA DIPLOMA KUANZIA MWAKA HUKU WA 2017/18"

Post a Comment

Loading...