Loading...
title : …Wabunge wakata posho kutoa rambirambi
link : …Wabunge wakata posho kutoa rambirambi
…Wabunge wakata posho kutoa rambirambi
Joyce Kasiki, Dodoma
OFISI ya Spika na Bunge la Jamhuri ya Muungano limetoa Sh milioni 100 kutoka posho za wabunge kwa ajili ya rambirambi kwa wazazi wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliopoteza maisha.
Wanafunzi hao walipoteza maisha Mei 6 wakati wakitoka Arusha kwenda Ngorongoro kufanya mtihani wa ujirani mwema kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya darasa la saba.
Mapema kabla ya kikao cha Bunge kuanza, Spika Job Ndugai aliwaongoza wabunge kusimama kwa dakika moja kuwakumbuka wanafunzi hao, walimu na dereva wao.
Akielezea utaratibu huo wa michango, Ndugai alisema wabunge hao walikubaliana kuwa kiasi hicho cha fedha kitagawiwa sawa kwa wafiwa wote.
Ndugai alisema rambirambi hizo za wabunge zilitolewa kwa makubaliano ya wabunge wote.
Hivyo makala …Wabunge wakata posho kutoa rambirambi
yaani makala yote …Wabunge wakata posho kutoa rambirambi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala …Wabunge wakata posho kutoa rambirambi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wabunge-wakata-posho-kutoa-rambirambi.html
0 Response to "…Wabunge wakata posho kutoa rambirambi"
Post a Comment