Loading...

Wenye vyeti bandia wakimbia madeni

Loading...
Wenye vyeti bandia wakimbia madeni - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wenye vyeti bandia wakimbia madeni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wenye vyeti bandia wakimbia madeni
link : Wenye vyeti bandia wakimbia madeni

soma pia


Wenye vyeti bandia wakimbia madeni


Mwandishi Wetu, Simiyu


SIKU chache baada ya Serikali kuweka hadharani majina ya watumishi wa umma wenye vyeti bandia, baadhi wameanza kukimbia madeni waliyokopa kwa watu binafsi, huku wategemezi wao wakikosa mahali pa kukimbilia.

Uchunguzi uliofanywa mkoani hapa umebaini kuwa baadhi ya watumishi wa umma hasa walimu waliokuwa wamekopa kwa watu binafsi, wameanza kukimbilia kusikojulikana, huku baadhi yao wakizima simu na kuhama makazi yao kimyakimya.

Mmoja wa wafanyabiashara wa Bariadi, Mashaka Magembe alisema amekuwa akikopesha walimu kwa riba, lakini baada ya kubaini kuwa baadhi yao wameondolewa kwenye utumishi wa umma kwa kuwa na vyeti bandia alianza kuwatafuta ili kulipwa madeni, lakini hakufanikiwa.

“Baada ya kuona majina yao kwenye orodha, niliwapigia simu lakini hawakunipa ushirikiano kama awali…mmoja nilikuwa namdai Sh 300,000, nilipompigia simu alisema tukutane mtaani badala ya nyumbani kwake na nilipofuatilia kwake nikakuta ameshahama,” alisema Magembe.

Aliongeza kuwa baadhi yao walirejesha fedha kidogo huku wakisema kuwa hali ni mbaya kulingana na majina yao kuwa kwenye orodha ya watumishi walioghushi vyeti huku wakiomba awasimamishie riba na watakuwa wanalipa kidogo kidogo.

Alisema hadi sasa hajui aliko mmoja wa wadeni wake wala simu yake haipatikani na ameshahama alikokuwa akiishi wakati kwenye mkataba wa mkopo aliweka dhamana ya seti ya sofa, televisheni, friji na kitanda.

Joel Peter ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tabora, alisema hatamalizia masomo yake kutokana na wategemezi wake wote kubainika kuwa na vyeti bandia.

Alisema kaka yake ambaye ni mwalimu wilayani Itilima amebainika kuwa na vyeti bandia, hivyo ana wasiwasi juu ya upatikanaji wa fedha za kumalizia masomo yake ya ualimu.

“Kaka na mkewe wote wamebainika kuwa na vyeti bandia na ndio walikuwa wakinisomesha, sasa sijui itakuwaje na wazazi wangu walishafariki dunia,” alisema Joel huku akiiomba Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi walio masomoni.

Habari zaidi zilieleza kuwa baada ya agizo la Rais John Magufuli kutaka watumishi wenye vyeti bandia kutoweka ofisini, baadhi ya maofisa utumishi mkoani hapa wameanza kutoa barua za kuwafukuza kazi watumishi hao mara moja.


Hivyo makala Wenye vyeti bandia wakimbia madeni

yaani makala yote Wenye vyeti bandia wakimbia madeni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wenye vyeti bandia wakimbia madeni mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wenye-vyeti-bandia-wakimbia-madeni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wenye vyeti bandia wakimbia madeni"

Post a Comment

Loading...