Loading...
title : WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU
link : WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU
WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WANAFUNZI wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa kupita katika Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kwa ajili ya kuangalia vigezo ambavyo vinahitajika.
Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje anatakiwa kuwa na ufaulu wa D mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa.
Amesema kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika tume hiyo ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu, akirudi anakuwa anakosa sifa katika mfumo wa elimu nchini.
Kwa upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali. Amesema India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.
Naye, Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa nchi ya India iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.
Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU kwa ajili ya kuhakikiwa..
Maonesho vya vyuo vikuu vya nchini India yamefadhiliwa a kampuni ya Global Education Link (GEL).
Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk.Fabian Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India Nchini Tanzania, Sandeep Arya akizungumza akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Nassor akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.Fabian Mahundu akiwa na Balozi wa India nchini, Sandeep Arya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakitembelea mabanda katika maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India.leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa India nchini, Sandeep Arya akiwa katika picha ya watanzania 25 waliopata ufadhili wa Serikali ya India wa kusoma katika vyuo vikuu vya nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU
yaani makala yote WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wanafunzi-wanokwenda-vyuo-vikuu-vya-nje.html
0 Response to "WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU"
Post a Comment