Loading...
title : Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi
link : Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi
Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi
Dalila Sharif
IGP Mangu |
WAKAZI wa Mtaa wa Mkondogwa, kata ya Chamanzi, Temeke wameliomba Jeshi la Polisi na Polisi Jamii kudhibiti ujambazi kwenye kituo cha mabasi cha Lulu mtaani humo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti jana, wakazi hao walisema matukio mengi ya ujambazi hutendeka eneo la kituo hicho na kuhatarisha maisha ya watu.
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Nassoro Lukindo alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kueleza kwamba matukio hayo yanafanyika kwenye mtaa wake kwa kutumia silaha za moto wakivamia maduka na kupora pesa.
“Vema walinzi shirikishi kujitokeza na kuendelea kuimarika katika mapambano ya kudhibiti uvamizi wa kutumia silaha na wezi na Jeshil la Polisi kutusaidia ili kuondoa uhalifu huo,” alisema Lukindo.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Hamidu Hamdu alisema hali si shwari kutokana na kukithiri uvamizi na kuwasababishia woga wakazi wa eneo hilo na abiria wanaotumia kituo wakihofia kuporwa na kuhatarisha maisha yao.
“Siku mbili zilizopita, kulitokea uvamizi wa uporaji wa kutumia silaha za moto na kuvamia baadhi ya maduka katika eneo hili, hali ambayo matukio haya hujirudia huku tukihofia usalama wetu,” alisema Hamdu.
Mary Johson wa mtaa huo alisema ni vema Jeshi la Polisi likaongeza ulinzi ili kudhibiti matukio hayo yanayotokea ili kuzinusuru mali na usalama wa maisha ya wakazi na wageni wa eneo hilo.
“Licha ya kuwa na Polisi Jamii haiwezi kusaidia pekee katika kudhibiti watu wanaotumia silaha ni vema kuwa na umoja katika kutoa taarifa mapema ili kudhibiti matukio hayo,” alisema Mary.
Hivyo makala Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi
yaani makala yote Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/waomba-polisi-kudhibiti-uhalifu-stendi.html
0 Response to "Waomba Polisi kudhibiti uhalifu stendi"
Post a Comment