Loading...

BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO

Loading...
BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO
link : BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO

soma pia


BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro amesema mwamko mdogo wa kielimu walionao Wananchi wengi ndio unaopelekea ongezeko kubwa la vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea kushuhudiwa kufanyika kila kukicha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Alisema baadhi ya Watu wakorofi wamekuwa wakitumia udhaifu huo kwa kuendeleza vitendo viovu dhidi ya Wanawake na Watoto ambao huathirika kiakili na kimwili na kuwapa wakati mgumu wa kuendelea na maisha yao ya kawaida ndani ya Jamii inayowazunguuka.
IGP Simon Sirro alieleza hayo wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.
Kamanda Sirro alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba katika kukabiliana na vitendo hivyo viovu vinavyoonekana kuleta fadhaa inalazimika kwa Jamii wakati huu kubadilika kwa kuwa tayari kutoa ushahidi pale wanaposhuhudia vitendo hivyo.
Alisema kesi yoyote inategemea kuendeshwa katika misingi na taratibu za Kisheria kwa kuzingatiwa ushahidi unaotolewa na mashahidi ili haki inapotolewa iende sambamba na stahiki ya pande zote husika.
Kamanda sirro aliitahadharisha Jamii inayopenda kulalamika zaidi kwamba nje ya kukosekana kwa ushahidi wa tuhuma zozote zinazowasilishwa Polisi na hatimae kwenye Ofisi ya Muendesha Mashtaka maana yake hakuna kesi itakayoendelea hata kama kuna mtu aliyedhulumiwa.
Alisema zipo kesi nyingi za udhalilishaji hasa zile za utelekezaji wa familia zinazofanywa na baadhi ya Wanaume zaidi upande wa Tanzania Bara zinazofikia zaidi ya asilimia 80% na kusababisha familia husika kukosa matunzo jambo ambalo huchangia ongezeko la Watoto wa Mitaani wanaokosa malezi ya Familia.

“ Tunafarajika kuona kwamba ipo Sheria ya adhabu dhidi ya Watu wanaotupa na kutelekeza Familia zao kwa upande wa Tanzania Bara ambayo imekuwa ikitumika na kupunguza matukio kama hayo ”. Alisema Kamnada Simon Sirro.

Akizungumzia hali ya Amani Nchini Tanzania Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Tanzania alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Nchi bado iko shwari licha ya matukio ya hapa na pale yanayoshuhudiwa katika Maeneo ya Rufiji.
IGP Sirro kupitia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi waendelee kushirikiana na vikosi vya ulinzi katika kutoa Taarifa za matukio ya uhalifu, Ujambazi na Uhujumu Uchumi kwenye maeneo yao ili vyombo vya Ulinzi vitumie maarifa yake katika kuwasaka wahalifu hao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisha Rasmi baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifafanua tatizo la Udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto linaloonekana kuathiri Jamii wakati akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro.


Hivyo makala BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO

yaani makala yote BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/balozi-seif-akutana-na-mkuu-wa-jeshi-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BALOZI SEIF AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO"

Post a Comment

Loading...