Loading...
title : CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO
link : CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO
CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO
NA mtumwa Ally
mwambawahabari
SHIRIKA la Utu wa Mtoto (CDF) limewataka wadau mbali mbali kwa kushirikiana na wazazi kushiriki kikamilifu katika kupambana kupinga ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kuwaozesha ndoa chini ya umri ya 18.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salam jana na Mkurugenzi Mtendaji Kashuma Mtengetii wa shirika hilo, alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia jitihada wanazozichukua katika kumpigania mtoto wa kike katika kupata haki zake za msingi ikiwemo kupata elimu sawa na mtoto wa kiume.
Alisema kuwa, licha ya jitihada mbali mbali wanazozichukua katika suala hilo kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali pamoja na wazazi lakini wameona bado inahitajika elim zaidi kwa kuwaelimisha wazazi juu ya athari wanazozipata watoto ambao wanaozeshwa ndoa za mapema.
"Sisi kama Shirika tumekua tukifanya jitihada mbali mbali za kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi ili kuweza kutimiza ndoto zao ,lakini changamoto kubwa tuliyoigundua ni elimu juu ya athari wanazozipata watoto hawa"alisema Kashuma.
Hata hivyo,alisema ripoti ya kitaifa iliyotolewa mwaka 2011 inaonesha kuwa watoto watatu kati ya 10 tayari wameshafanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kuozeshwa ndoa za mapema jambo ambalo linarudisha nyuma harakati za maendeleo kwa watoto hao.
Aliongeza kuwa,kutokana na sababu mbali mbali zinazopelekea kukua kwa tatizo hilo ikiwemo umaskini,thamani ya mtoto wa kike pamoja na ile sheria inayoruhusu watoto kuolewa chini ya umri wa miaka 18 ipo haja ya wadau kukutana pamoja ili kuweza kutokomeza jambo hili.
Kashuma alisema ,mtoto wa kike kumuozesha Mume akiwa na umri mdogo kunamsababishia madhara makubwa anayoyapata ikiwemo kukatisha shule, kuweza kupata matatizo ya kiafya pamoja na kufariki jambo ambalo linakatiza ndoto na matumaini katika maisha yao.
Alisema kuwa,licha ya takwim za mwaka 2016/17 kuonesha tatizo la ndoa za utotoni zimepungua kwa asilimia 1 lakini bado ni changamoto nchini Tanzania hususani Vijijini ikilinganishwa na mjini.
"Tatizo hili bado nchini kwetu ni changamoto kubwa kubwa husasani maeneo ya vijini ambapo huku imekua ni rahisi wazazi kuweza kukubali kuwaozesha watoto wao ndoa za mapema ikilinganishwa na mjini"alisema Kashuma.
Mwishoo.
Hivyo makala CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO
yaani makala yote CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/cdf-yawataka-wadau-kushirikiana-na.html
0 Response to "CDF YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO"
Post a Comment