Loading...

DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Loading...
DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI
link : DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

soma pia


DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kazi za kizalendo anazoendelea kuzifanya kwa maslahi mapana ya Taifa .

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Mhandisi John Jeremiah amesema wanaunga mkono jinsi suala la mchanga wa madini (makinikia) linavyoshughulikiwa na Serikali ikiwa ni moja ya hatua za kuleta mageuzi ya kweli na kujenga Tanzania mpya.

“Tofauti na wale wanasiasa wanaobeza juhudi za Rais Mgufuli sisi wana DARUSO tunapenda kumuhakikishia kuwa tuko pamoja nae kifikra, kimikakati na kimaombi na tunaamini kuwa fedha iliyopaswa kulipwa na ACACIA kwa Tanzania tangu 1998 hadi 2017 zitalipwa mara moja”Alisisitiza Jeremiah.

Aliongeza kuwa ripoti ya kamati iliyoongozwa na Profesa Michael Ossoro imebainisha kuwa fedha zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu hivyo juhudi za kulinda rasilimali za Taifa zinapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania 

“DARUSO tunapenda kukumbusha kuwa vita hii sio ya chama chochote cha siasa bali ni vita ya watanzania wote kwa hivyo tusimame na kuungana na Mhe. Rais wetu Dkt. Magufuli kwenye mapambano haya.” Alisisitiza Mhandisi Jeremiah

Mwandisi Jeremiah amesema kuwa kiwango hicho cha fedha kingetosha kuhudumia huduma za kijamii hivyo kuwapa Watanzania unafuu wa maisha.  

“Tunapenda kumpongeza Mhe. Rais kwa muelekeo mzuri wa juhudi zake za kizalendo zilizomfanya Mwenyekti Mtendaji wa Kampuni ya (Afica) Barrick Gold Mining Professor John Thornton kuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu”.Alisisitiza Mwandisi Jeremiah.
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Mhandisi John Jilili(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kupongeza juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli. Kulia ni Makamu wa Rais wa Serikali hiyo bi Anastazia Anthony na kushoto ni Waziri wa michezo,Haiba na Burudani Bw. Mabina David. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
  (Picha na frank Mvungi-MAELEZO)


Hivyo makala DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

yaani makala yote DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/daruso-yampongeza-rais-magufuli.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI"

Post a Comment

Loading...