Loading...

DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI

Loading...
DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI
link : DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI

soma pia


DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI

*Ni zile korofi na zilizoharibiwa na mvua
*Amkabidhi mhandisi wa manispaa mitambo ya kazi,lita 10,000 za dizeli

Wilaya ya Kinondoni leo imezindua ukarabati wa barabara zenye urefu wa Kilomita 148 ambazo zimeharibiwa na mvua zilizonyesha katika msimu uliopita hali iliyosababisha adha ya usumbufu na foleni kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi ameeleza hayo wakati akizindua matengenezo hayo na kumkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni ambaye pia ni mhandisi wa manispaa hiyo Abdul Digaga mitambo ya ujenzi wa barabara na lita 10,000 za dizeli.

Mafuta na mitambo hiyo inatokana na juhudi za Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na wadau wa kampuni za TOTAL TANZANIA na kampuni ya ujenzi GRAND TECH zilizotoa mitambo na mafuta ya dizeli kama sehemu ya mchango wao kwa DC Hapi kwa juhudi zake na za serikali ya awamu ya tano kwa ujumla katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Kinondoni.

Barabara zitakazofanyiwa ukarabati ni barabara zote korofi na zilizoharibiwa na mvua katika kata zote 20 za manispaa ya Kinondoni.

Aidha, DC Hapi ametembelea ujenzi wa barabara ya Nzasa KM 1.2 kwa kiwango cha lami unaofanywa na kampuni ya Esteem chini ya mradi wa Uboreshaji jiji la Dar es salaam (DMDP) ambapo chini ya mradi huo wilaya ya Kinondoni itanufaika na kiasi cha bilioni 22 huku Mfuko wa barabara ikiwa na bilioni 6 zilizoruhusiwa kutumika kukamilisha miradi iliyosimamishwa ya 2016/2017.

"Mbali na juhudi hizi za wadau waliojitolea kunisaidia mafuta na mitambo ya kutengenezea barabara, tunazo bilioni 6 za Mfuko wa barabara na tutanufaika na bilioni 22 za mradi wa Uboreshaji wa jiji la Dar es Salaam.Hivyo wananchi msiwe na wasiwasi, mwaka huu ujao wa fedha ni mwaka wa barabara kwa Kinondoni." Alisema Hapi.

DC Hapi aliwaomba wananchi waliojitokeza kuendelea kumuombea Rais Dr. John Magufuli na wasaidizi wake wote kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo nchini.

Uzinduzi wa ukarabati huo wa barabara umefanyika katika kata ya Kijitonyama na kuhudhuriwa na wananchi wa eneo hilo.


Hivyo makala DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI

yaani makala yote DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/dc-hapi-azindua-ukarabati-wa-barabara.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC HAPI AZINDUA UKARABATI WA BARABARA MBOVU KINONDONI"

Post a Comment

Loading...