Loading...

DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI

Loading...
DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI
link : DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI

soma pia


DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI

MKUU1
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya kufanya kushtukiza katika kiwanda cha plastic cha Ruider Plastic Limited kinachomilikiwa na raia mwenye asili ya China wilayani Kigamboni.
MKUU2
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa akifanya ukaguzi mara baada ya ziara ya kufanya kushtukiza katika kiwanda cha plastic cha Ruider Plastic Limited kinachomilikiwa na raia mwenye asili ya China wilayani Kigamboni.
MKUU3
Hizi ni baadhi ya bidhaa mbalimbali zinazozaliswa na kiwanda hicho kinyemela.
…………………………………………………………………………………
Ni kufuatia ukwepaji wa kodi za serikali…
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, leo tarehe 20/7/2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha plastic cha Ruider Plastic Limited kinachomilikiwa na raia mwenye asili ya China.
DC Mgandilwa aliyeambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Steven Katemba, walikagua na kugundua mambo mbalimbali yakiwemo ya kiwanda hicho kuendesha shughuli zake pasipo kufuata taratibu za nchi kikamilifu na baadhi ya mianya ya ukwepaji wa kodi.
Baada ya kutembelea eneo la kiwanda ili kujionea shughuli za uzalishaji, Msafara huo ulioongozwa na DC Mgandilwa ulibaini kuwa katika eneo hilo kuna viwanda tofauti Saba vinavyozalisha bidhaa tofauti tofauti.
Viwanda vilivyobainika ni pamoja na kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji ya plastic, kiwanda cha kutengeneza mikeka, kiwanda cha kutengeneza bodi za dari (Ceiling board), kiwanda cha kutengeneza mifuko ya plastic, kiwanda cha kutengeneza maboksi ya plastic kwa ajili ya kutunza vitu vya baridi, kiwanda cha kuyeyusha chupa za plastic, na kiwanda cha kutengeneza mito ya kulalia.
Viwanda vyote hivyo Saba vinafanya shughuli za uzalishaji katika eneo moja na huku kiwanda kinacholipa kodi za serikali kikiwa ni kimoja tu nacho kikisuasua kulipa kama inavyostahili.
Baada ya kutembelea viwanda vyote hivyo, DC Mgandilwa amewataka wamiliki wa viwanda hivyo kusitisha uzalishaji wake mara moja leo hii.
DC Mgandilwa amesema kusimama kwa shughuli za uzalishaji unatoa mwanya kwa timu kutoka mamlaka ya mapato (TRA) na Manispaa ya Kigamboni ambao amewaagiza kuweka kambi katika viwanda hivyo kuanzia kesho ili kupitia nyaraka zote na kubaini kiasi cha mapato ambayo serikali imekuwa ikiyapoteza tangu waanze uzalishaji.
DC Mgandilwa ameagiza kuwa baada ya tathimini hiyo kukamilika pesa yote ambayo serikali imekuwa ikipoteza tangu kuanzishwa kwa viwanda hivyo ilipwe mara moja iwezekanavyo na ndipo uzalishaji uendelee kwa kufuata taratibu zote za serikali.
Inakadiriwa kuwa kiwanda kimoja kilitakiwa kulipa Shilingi Milioni 101kwa mwezi hivyo kuifanya serikali kupoteza mapato ya zaidi ya Shilingi Milioni 700 kwa mwezi kwa viwanda vyote.


Hivyo makala DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI

yaani makala yote DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/dc-mgandilwa-afunga-viwanda-vya-wachina.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC MGANDILWA AFUNGA VIWANDA VYA WACHINA KIGAMBONI"

Post a Comment

Loading...