Loading...

HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT

Loading...
HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT
link : HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT

soma pia


HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe awashukuru BAY PORT Taasisi ya kifedha kwa msaada wa kompyuta mbili walizozitoa Jana kwa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu..

Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa anashukuru kwa msaada wa kumpyuta hizo ambazo zitakwenda kwenye Idara ya Utumishi na Rasilimali watu ili kuimarisha Idara na ufanisi wa Idara hiyo kwa kuzingatia unyeti wa eneo hilo na huduma wanayoitoa kwa watumishi.

Miongoni mwa Halmashauri 80 ambazo zimelenga kufikiwa na BAYPORT tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekuwa moja wapo na tunaahidi kutumia vifaa hivi vya TEHAMA kwa kuongeza ufanisi na utendaji kazi ulioboreka zaidi.

Mratibu wa masoko na mawasiliano wa huduma za kifedha za BAYPORT Mercy Ndunguru alisema kuwa BAYPORT imeamua kurudisha faida ambayo wameipata ambapo kwa sasa wameona waguse sekta ya utumishi ambayo imekuwa na msaada mkubwa katika kufikia malengo.

Mercy alisema kuwa, Tunaamini kwa kutoa vifaa hivi vya TEHAMA itasaidia kuongeza ufanisi kwenye sekta ya utumishi na watumishi watapata huduma kwa wakati, BAYPORT inamuunga mkono Raisi kwenye utendaji kazi kwa watumishi.

Meneja wa BAYPORT Handeni Kanji Masanji alisema kuwa, anashukuru kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kwamba taasisi yao inajipanga kufanya mambo mengine makubwa zaidi ya haya ikiwa ni pamoja na kujipanga kufadhili timu mbalimbali za mipira na kuinua vipaji vya vijana waliopo Wilayani Handeni.

BAYPORT wametoa msaada huo wa kompyuta mbili ikiwa ni miongoni mwa kompyuta zenye thamani ya zaidi ya milioni 500 zinazoendelea kutolewa kwenye taasisi nyingine za Kiserikali.

Alda Sadango

Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
Afisa utumishi Wilaya Noel Abel akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ambapo kushoto ni Afisa utumishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kulia ni Mratibu wa masoko na mahusiano na meneja wa tawi LA BAYPORT Handeni


Hivyo makala HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT

yaani makala yote HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/halmashauri-wilaya-ya-handeni-yapigwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "HALMASHAURI WILAYA YA HANDENI YAPIGWA JEKI KOMPYUTA MBILI NA BAYPORT"

Post a Comment

Loading...