Loading...
title : JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH
link : JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH
JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH
Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,dk.John Magufuli ,ametoa wiki moja kwa wizara ya fedha kutoa kiasi cha sh .Bil .1.3 ,kwa ajili ya kuondoa zaidi ya lita 100,000 za madawa ya viatilifu vya viuadudu vya mazalia ya mbu ,zilizokosa soko katika kiwanda cha Biotech Products Limited,kilichopo Mji Wa Kibaha ,Pwani .
Aidha ameeleza agizo hilo litaenda pamoja na maelekezo atakayoyatoa kwa kila halmashauri ikatwe kiasi gani katika fedha hizo .
Dk.Magufuli amewataka wakurugenzi wa halmashauri nchini kila mmoja aanze kupanga ratiba yake ya kwenda kuchukua akiba yake ya madawa ambayo yatakuwa kwenye utaratibu kwa kila halmashauri .
Amekitaka pia kiwanda hicho kijitangaze katika vyombo mbalimbali vya habari na kutoa elimu kwa jamii kuwa madawa hayo hayana madhara kwa matumizi ya binadamu .
Hayo aliyasema ,wakati alipokwenda kutembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited katika ziara yake ya kikazi ya siku ya tatu mkoani Pwani ,ambapo ni hatima ya ziara hiyo .
Anasema kiwanda hicho tangu kifunguliwe na rais mstaafu Wa awamu ya nne dk.Jakaya Kikwete dawa zinatengenezwa na kujazana bila kununuliwa .
Dk.Magufuli ,alieleza kuwa ,serikali inatumia mabilioni ya fedha kununua madawa ikiwa ni pamoja na mwaka 2015 serikali ilitenga bil. 31 na mwaka 2016 na 2017 serikali imetenga bil.250 .
""Mzalishe na kufanyakazi zenu, pasipo kuchakachua ubora uliopo ,kisa kupata soko ,nataka nione ugonjwa wa malaria unamalizika baada ya muda na wagonjwa wanapungua mahospitalini " alisema dk .Magufuli .
Alieleza lengo kuu ni kuondoa ugonjwa Wa malaria kama ilivyo Zanzibar .
Dk .Magufuli ,alisema wananchi wanapaswa wanunue madawa hayo ili kujikinga na kumaliza ugonjwa huo ,hapa nchini.
Alibainisha kwamba ,ni maajabu nchi za nje na Niger ,wananunua madawa hayo nchini Tanzania huku watanzania kushindwa kununua bidhaa zinazozalishwa hapa.
Nae kaimu Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Samwel Mziray ,alisema halmashauri nyingi bado hazijanunua dawa hizo ili kutimiza malengo ya serikali .
Mziray alisema awali ilielekezwa madawa yanayozalishwa ilikuwa ni jukumu la wizara ya afya kuzinunua kisha kuzisambaza kwenye halmashauri nchini ambapo ilijiengua .
"Tatizo hapa ni oda ,tukitengeneza madawa mengi yana muda ,inatakiwa yakishazalishwa yatumike ili kuzalisha mengine " alisema .
Mziray ,alisema kwasasa wanazalisha lita 48,000 za dawa kwa wiki na kuuza kwa sh .13,000 kwa lita .
Hivyo makala JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH
yaani makala yote JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/jpm-aokoa-madawa-yaliyokosa-soko-katika.html
0 Response to "JPM -AOKOA MADAWA YALIYOKOSA SOKO KATIKA KIWANDA CHA BIOTECH"
Post a Comment