Loading...
title : Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili
link : Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili
Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeshiriki katika madhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu duniani kwa kuendesha shughuli ya utoaji damu kwa watu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wenye uhitaji.
Shughuli hiyo inaendelea katika hospitali hiyo kwenye Jengo la Maabara kuu ambako watu wamekusanyika kwa ajili ya kuchangia damu. Mmoja wa viongozi walishriki katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema pamoja na Watanzania mbalimbali.
Akizungumza katika shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo wakiwamo kinamama na watoto wadogo.
“Nawapongeza wote walifika leo hapa Hospitali ya Muhimbili kuchangia damu, ni jambo la muhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa,” amesema Mheshimiwa Mjema.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa hospitali hiyo, Dk Praxeda Ogweyo amewataka wananchi,mashirika ya umma na yasiyo ya kiserikali, shule, vyuo mbalimbali na taasisi za dini kujitokeza kuchangia damu hospitali hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Njema akizungumza na Jonas Hans Atile (kushoto) ambaye amejitokeza kuchangia Damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Praxeda Ogweyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani. Pia Dk. Ogweyo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
Mmoja wa Wananchi akishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu duniani Leo katika hospitali hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili
yaani makala yote Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/maadhimisho-ya-siku-ya-kuchangia-damu.html
0 Response to "Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili"
Post a Comment