Loading...
title : Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni.
link : Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni.
Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni.
Na: Lilian Lundo
Serikali inatarajia kutoa huduma za ukatishaji wa tiketi kwa njia ya mfumo wa kielekroniki katika kivuko cha Magogoni ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela.
Akiongea na Maelezo Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dkt. Musa Mgwatu alisema kukamilika kwa mfumo huo utakaogharimu bilioni 1.1 kutasaidia kuiongezea mapato serikali kwani mfumo huo utafanyakazi kwa njia za kielekroniki.
“Ujenzi wa mashine za kielektroniki umeshaanza na kukamilika kwa upande wa magogoni, Mkandarasi anatarajia kuanza ufungaji wa mashine hizo upande wa Kigamboni wiki hii,” alifafanua Dkt. Mgwatu.
Dkt. Mgwatu alisema Mkandarasi wa mradi huo anatarajia kukamilisha uwekaji wa mashine hizo julai 25 mwaka huu na utumiaji wa mashine hizo utaanza kutumika tu mara baada ya makabidhiano kutoka kwa mkandarasi.
Akizungumzia gharama za kuvuka Dkt. Mgwatu amesema, gharama za kuvuka zitabaki pale pale na hakutakuwa na ongezeko lolote mashine hizo zitakapoanza kutumika.
Bwana Ismail Juma, mkazi wa Kigamboni amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kumekuja wakati muafaka na kutasaidia kuiongezea mapato serikali na kuepusha upotevu wa mapato katika vivuko hivyo.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano aliwaagiza TEMESA kufunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao utadhibiti ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato.
Hivyo makala Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni.
yaani makala yote Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mashine-za-kielektroniki-kuanza.html
0 Response to "Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni."
Post a Comment