Loading...

Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika

Loading...
Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika
link : Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika

soma pia


Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika


Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo. 

JUNI 16, 2017: Dar es Salaam, Tanzania. Katika maadhimisho ya Siku yaMtoto wa Afrika mwaka huu mtoto mwenye umri wa miaka sita Ethan Theodore Yona anayesoma darasa la kwanza amezindua zana(App) yake ya android ambayo inaonesha shujaa wa hali ya juu akiwa ni muhusika anayejulikana kama EthanMan. Mhusika anaegemea upande wake ni mwenye kipaji kikubwa, ameandika vitabu vya kuvutia, kubuni michezo ya kijifunza na kuwapelekea watoto katika safari za mafunzo.

Ethan alianza kujishughulisha na mradi huo alipokuwa na umri wa miaka mitano katika shule ya awali ikiwa ni matokeo ya mapenzi yake katika michezo na kujifunza. “Kila mara nilikuwa na nguvu , kufurahia kujifunza vitu vipya na kupenda kucheza michezo mbalimbali. Siku moja niliwaambia wazazi wangu ningependa kuanzisha mhusika mkuu jasiri kwa kuzingatia ubora wangu. 


Baadaye waliniuliza ubora huo ni upi na nikawaambia mimi ninakipaji kikubwa na ninaweza kuwa kitu chochote ninachokipenda , naweza kuwa mchezaji soka, nyota wa muziki, mhandisi n.k. Na hivyo ndivyo wazo la mhusika shujaa mkuu lilivyoanza.”
 

Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo. 


Ethan alifanya kazi hiyo na mshauri wa teknolojia ya elimu katika i-LearnEast Africa, na ambayo inatoa kozi kwa njia ya mtandao na mafunzo ya mabadiliko kuunda mhusika huyo na kuanzisha kitabu chake cha kwanza cha picha alichokiita “Nitakapokuwa Mkubwa”. Tulivutiwa sana kufanya kazi na Ethan katika mradi huu. 


Inafurahisha kwamba mtoto mdogo namna hii kutaka kufanya jambo hili kubwa tulitaka kuwa sehemu ya huu mradi tangu mwanzo. Ikiwa ni kampuni ya ushauri katika masuala ya elimu tuliona umuhimu wa kujifunza ambao mradi huu utawapatia watoto. Mchango wa Ethan katika kuandaa kitabu hiki ni wa kushangaza,” alisema Ofisa Mtendaji wa Learn Tech, Deus Ntukamanzina. 


Zana hiyo na michezo ilianzishwa kwa ushirikiana na kampuni ya Tujenge Technology ambayo imejikita katika kuanzisha masuluhisho ya kidijitali ambayo yatawezesha kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.
 
Mtoto Ethan Thedore Yona akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kwa njia ya mtandao(App) kijulikanacho kama Ethan Man, hafla hiyo imefanyika leo kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam. 


“Tulipoombwa kuanzisha michezo ya EthanMan tulifurahi. Kuwa sehemu ya mradi huu wa kipekee ndicho kilichotufanya kuingia katika teknolojia na kuianzisha. Mchango wetu ilikuwa ni kuunganisha mhusika EthanMan na vipaji vyake vingi katika jukwaa ambalo itakuwa ni rahisi kufikiwa na kuanzisha uzoefu mkubwa wa kutumia miongoni mwa watoto. Mchango wa ethan katika kuanzisha michezo ni wa hali ya juu, kwa sababu kila kitu kimejielekeza katika maisha yake kama mhusika. Tulikuwa na muda mzuri wa wa kuunda kile ambacho tunaamini kuwa ni bidhaa ya kwanza ya mchezo katika anga ya teknolojia nchini Tanzania.

Zana (App) ya EthnMan inapatikana kwa kupakua katika hifadhi ya michezo ya android , watoto wataweza kusoma vitabu, kucheza michezo. Na kuwa pamoja na muundaji wa EthanMan, Ethan Theodore Yona.


Hivyo makala Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika

yaani makala yote Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mtoto-wa-miaka-sita-darasa-la-kwanza_16.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika"

Post a Comment

Loading...