Loading...

Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe

Loading...
Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe
link : Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe

soma pia


Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na watendaji wake kuhakikisha Mji wa Kisarawe uliopo mkoani Pwani unapata huduma ya maji safi na salama.

Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo jana mkoani Pwani wakati akizindua Mradi wa upanuzi wa Mtambo wa  maji wa Ruvu Juu na ulazaji wa Mabomba Makuu kutoka Mlandizi kwenda Jijini Dar es Salaam.

Mh. Magufuli amesema kuwa Mkoa wa Pwani umefanya kazi kubwa ya kutunza miundombinu ya maji ambayo imewezesha kuhudumia wananchi wa Dar es Salaam hivyo ni haki kwa wananchi wa Mkoa huo kufaidika na maji wanayoyatunza kwa muda mrefu.

“Ninafahamu Mji wa Kibaha kwa sasa hauna shida ya maji, shida iliyopo ni kuzidi kwa presha ya maji ambayo sio tatizo la DAWASA wala DAWASCO hivyo ili kutatua tatizo hilo ni jukumu la Wizara husika na watendaji wake kujipanga na wahandisi wa maji kuunganisha bomba kutoka Wilaya ya Kibaha hadi Kisarawe ambapo kuna changamoto ya maji safi na salama,” alisema Rais Magufuli.

Akiongelea utunzaji wa miundombinu ya maji, Rais Dkt. Magufuli amewataka watendaji wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhakikisha wanashughulikia maji yanayopotea kwa kurekebisha miundombinu ambayo imeharibika na kuweka miundo mbinu mipya inayoweza kuhimili wingi wa maji.

Aidha, Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa trilioni 1.3 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji kwa Miji 16 nchini ambayo ikikamilika itawezesha wananchi wengi kupata maji safi na salama hivyo amewaahidi kudumisha ushirikiano uliopo katika sekta ya maji baina ya nchi hizo mbili.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli


Hivyo makala Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe

yaani makala yote Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/rais-magufuli-amtaka-waziri-lwenge.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rais Magufuli Amtaka Waziri Lwenge Kuhakikisha Maji Yanapatikana kisarawe"

Post a Comment

Loading...