Loading...

Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars

Loading...
Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars
link : Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars

soma pia


Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars



Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Sammata ameihakikishia kampuni ya Bia ya Serengeti ambayo ni wadhamini wa timu ya taifa Taifa Stars kwamba wachezaji wa timu hiyo watajituma ili kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zote walizopangiwa kwenye ratiba.

Samatta ambaye ni nahodha wa timu hiyo ya taifa alitoa hakikisho hilo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuhudhuriwa na Meneja Masoko wa SBL, Nicholus Machugu. Mkutano huo ulijadili mechi kati ya Taifa Stars na Lesotho timu ambayo Stars inatarajiwa kucheza nayo katika mashindano yajayo.Alithibitisha kuwa timu hiyo haitaiangusha SBL katika mechi zake kwa kuwa kampuni hiyo imeonesha kuithamini kutokana na udhamini wake kwa timu hiyo.

Aidha alitoa wito kwa wachezaji wenzake kuhakikisha kuwa wanajiweka vizuri kkwa ajili ya mechi hizo ili waweze kuingia na kutambuliwa katika ramani ya soka barani Afrika.

Samatta ambaye hivi sasa anafanya shughuli zake kama mchezji wa kulipwa nchini Ubeljiji aliinga jijini Dar es Salaam Jumatano ya wiki hii ili kuungana na wachezaji wenzake wa timu ya taifa kwa ajili ya mechi ya duru ya kwanza ya kufuzu mashindano Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Duru ya pili ya mashindano hayo itafanyika Januari 2018 na mechi ya fainali inatarajiwa kufanyika kufanyika Cameroon mwka 2019.

Kwa upande wake Kocha wa Timu hiyo Salum Mayanga alisema kwamba timu yake imejitayarisha sawasawa kwa ajili ya mechi zote na kuongeza kuwa mazoezi ya timu hiyo iliyoyafanya walipokuwa Alexandria, Misri walikokuwa hivi karibuni hivi karibuni yaliwapa mwanga na ana matarajio makubw kwamba timu hiyo itashinda mechi zote.

Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ni mashindano ni mashindano makubwa ya kimatiafa barani Afrika. Mashindano hayo yalianzishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1957.

Kuanzia mwaka 1967, yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili. Wanachama wa Mashirikisho ya Soka ya FIFA ndio walio na sifa za kushiriki mashindano hayo.

Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania na Nahodha wa Taifa stars Mbwana Sammata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema m mwishoni wa wiki iliyopita kuhusu maandalizi yao ya kucheza na Lesotho katika mkutano na waandishi uliofanyika katika makao makuu ya TFF .

Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema mwishoni mwa wiki iliyopita. 


Hivyo makala Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars

yaani makala yote Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/samatta-apongeza-udhamini-wa-sbl-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa Stars"

Post a Comment

Loading...