Loading...
title : UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo
link : UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo
UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi.Salama Aboud Talib akiwahutubia viongozi wapya wa Matawi ya Majimbo ya Chaani na Mkwajuni Kaskazini “A” kichama Unguja.
Katibu wa Idara ya Organaizesheni wa UWT Zanzibar, Tunu Juma Kondo akizungumza na viongozi hao kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi.Salama Aboud Talib huko Gamba Ofisi ya Wilaya Kaskazini “A” Gamba Unguja.
Baadhi ya viongozi mbali mbali UWT wa ngazi za matawi wa Majimbo ya Chaani na Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini “A” wakifuatilia kwa makini nasaha zinazotolewa katika Mkutano huo.
mmoja wa Viongozi wa Tawi la Chaani Mcheza Shauri Bi. Fatma akitoa akizungumza katika Mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu Bi. Salama Aboud kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Viti Maalum Wilaya ya Kaskazini “A” Bi. Mtumwa Suleiman sadaka ya fedha kwa Akina Mama wa UWT kwa ajili ya futari ya Mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mwakilishi wa Viti Maalum Wilaya ya Kaskazini “A” Bi. Mtumwa Suleiman akigawa sadaka ya fedha kwa Akina Mama wa UWT kwa ajili ya futari ya Mwezi mtukufu wa ramadhani.NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), umewataka viongozi waliochaguliwa kwa ngazi za matawi ya umoja huo na chama kwa ujumla kuongeza idadi ya wanachama hai watakaoiwezesha CCM kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi. Salama Aboud Talib katika ziara ya kuwapongeza na kuwahamasisha viongozi wapya wa ngazi za matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika Majimbo ya Chaani na Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
Alifafanua kuwa viongozi hao wanatakiwa kujua idadi kamili ya wanachama na kubaini ni wanachama wangapi wamefariki ili watolewe katika orodha ya wanachama hai kwa lengo la kupata idadi ya uhakika ya wanachama watakaoendelea kuibeba CCM katika michakato mbali mbali ya kisiasa.
Alisema viongozi waliochaguliwa wameaminiwa hivyo wanatakiwa kuwatumikia na kuwaongoza vizuri wanachama waliowachagua kwa kutetea maslahi ya CCM kwa vitendo.
Aidha Aliwataka wanawake hao kuwa na masimamo imara wa kuendelea kuwachagua viongozi wenye sifa na uwezo wa kuzitumikia chama na jumuiya kwa uadilifu badala ya kuwatumikia watu wachache wenye nguvu za kisiasa na uwezo wa kifedha.
“Kuweni na msimamo na msikubali kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi nyinyi chagueni watu mnaowaamini kuwa watakuongozeni vizuri na kusimamia kwa uadilifu Chama chetu.
Pia Sote ni binadamu na uongozi ni jukumu zito lakini naamini kama tutashirikiana kwa kila hatua kazi zetu zitakuwa rahisi na chama chetu kitaendelea kung’ara na kuongoza dola”, alisema Bi.Salama.
Hata hivyo kupitia ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu huyo amesisitiza kudumishwa dhana ya umoja ndani ya jumuiya hiyo ili wasimamie ipasavyo matakwa ya Katiba ya CCM na Jumuiya waweze kufanikisha majukumu mbali mbali ya kuendelezwa kwa dhana ya umoja na mshikamano ndani ya jumuiya hiyo .
Naye Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini “A” kichama, Ame Omar Mkadam alisema Wilaya hiyo imefanikisha kwa ufanisi zoezi la uchaguzi kwa ngazi za matawi na kwa sasa wanaendelea kujipanga na ngazi za Wadi na majimbo ili nazo zifanishe zoezi hilo kwa ufanisi.
Naye Bi.Fatma Khamis mussa kutoka Tawi la Chaani, amewasihi viongozi wa ngazi za juu wa umoja huo pamoja na Chama Cha Mapinduzi kufanya ziara za mara kwa mara katika ngazi za Matawi ili kuongeza hamasa ushirikiano kwa wanachama na viongozi wa ngazi hizo.
Pamoja na hayo katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu huyo Bi. Salama Aboud kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Bi. Mtumwa Suleiman wametoa sadaka ya fedha kwa akina Mama wa UWT kwa ajili ya futari ya Mwezi mtukufu wa ramadhani.
Hivyo makala UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo
yaani makala yote UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/uwt-zanzibar-yashusha-majukumu-kwa.html
0 Response to "UWT Zanzibar yashusha majukumu kwa viongozi wapya wa matawi ya umoja huo"
Post a Comment