Loading...

SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI

Loading...
SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI
link : SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI

soma pia


SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI

Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma 

Serikali imewashauri wakazi wa Wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro, kutumia njia mbadala kupata huduma za kibenki ikiwemo kupitia simu za mkononi yaani (simbanking) ya CRDB na Banking on the Wheel ya NMB iliyoko Mlimba kwa kipindi hiki ambacho mchakato wa kufungua matawi rasmi ya benki unaendelea. 

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Malinyi Dkt. Hadji Hussein Mponda (CCM), aliyetaka kujua ni lini huduma rasmi za kibenki zitaanzishwa katika wilaya ya Malinyi ama kama kulikuwa na mpango wa taasisi za fedha kuanzisha huduma za matawi ya benki yanayohamishika (mobile banking) wilayani humo.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, wilaya ya Malinyi ni moja ya wilaya ambazo zinanufaika na mfumo wa utoaji huduma kupitia mawakala wa Fahari Huduma (Malinyi SACCOS na Zidua Waziri Shop) zinazoendeshwa na benki ya ‘CRDB Bank’ ambapo wateja wanapata huduma za kibenki ikiwemo kufungua akaunti, kuweka na kuchukua fedha, kuomba mikopo na kupata ushauri wa huduma za kifedha. 

“Gharama za kuanzisha na kuendesha tawi kuwa kubwa Benki ya NMB na CRDB zinaendelea na upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufungua tawi katika wilaya ya Malinyi utakaotoa mwelekeo wa kufungua tawi au la, kwa sababu Tawi linatakiwa liwe endelevu na kujiendesha kwa faida”. Alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wananchi wa Tanzania kupata huduma za kibenki karibu na maeneo yao na kwamba huduma hizo lazima ziwe na faida kwa pande zote yaani kwa mabenki na wateja pia. 



Hivyo makala SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI

yaani makala yote SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/serikali-yawashauri-wananchi-kutumia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAWASHAURI WANANCHI KUTUMIA NJIA MBADALA YA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI"

Post a Comment

Loading...