Loading...
title : TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma
link : TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma
TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma
Wakuu wa Idara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakijadili masuala mbalimbali walipotembelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Ramadhan Maleta, katika mwanzo wa Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23 kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhani Maleta akimsikiliza na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw.Joseph Nyahende (kushoto), wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 hadi 23. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu, Bw. Mohamed Ally na kushoto ni Mkurugenzi Viwanja vya Mikoa, Bw. Valentine Kadeha.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama katika jengo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri la VIP kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Leonard Mbogoma (wapili kushoto)akimuelezea jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta alipotembelea jengo hilo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Joseph Nyahende akimfafanulia jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta ikiwa ni siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
Ofisa Biashara wa JNIA, Bi. Herrieth Nyarusi (kushoto) akizungumza wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta alipotembelea Idara ya Biashara kusikiliza kero na maoni kutoka kwa watumishi, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Meneja wa Fedha (JNIA), Bw.Shadrack Chilongani na katikati ni Bw. Godfrey Kanyama.
Hivyo makala TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma
yaani makala yote TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/taa-yaanza-wiki-ya-utumishi-wa-umma.html
0 Response to "TAA yaanza Wiki ya utumishi wa Umma"
Post a Comment