Loading...
title : TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR
link : TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR
TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR
23/06/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El Fitri, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao. Kipindi kama hiki cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi nchini, limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba wananchi wanasherehekea Sikukuu katika hali ya amani na utulivu.
Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Vilevile, Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunja sheria na kanuni za usalama barabarani kwa mabereva kutumia vilevi, bodaboda kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi pamoja na kupiga honi hovyo.
Pia, tunawataka wananchi wote kuwa wepesi katika kutoa taarifa kwa kupitia namba za simu za bure 111 au 112 pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara.
Tunawatakia watanzania wote Sikukuu njema ya Eid El Fitri.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba -ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
Hivyo makala TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR
yaani makala yote TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/taarifa-ya-jeshi-la-polisi-tahadahari.html
0 Response to "TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR"
Post a Comment