Loading...
title : TAARIFA YA MSIBA
link : TAARIFA YA MSIBA
TAARIFA YA MSIBA
Familia ya Bw. Byabato wa Kinondoni, Morroco Dar es salaam inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Bw. Francis Byabato kilichotokea tar 12 June katika hospitali ya Muhimbili Dar es salaam. Miaka ya Awali, Marehemu alifanya kazi na kampuni ya East African Community Nairobi na Arusha, na katika ofisi ya Hazina ( Treasury) Dar es salaam. Baada ya kustaafu alianzisha biashara kampuni ya Bureau de Change jijini Dar es salam.
Marehemu ameacha Mke wake Mpendwa. Demetria Byabato wa Kinondoni, Dar es salaam, pamoja na wanae --Digna Byabato- Makobore (Daudi) wa Mikocheni, Dar es salaam, Alvera Byabato- Ijumba (Edmund) wa Memphis, Tennessee, Hilda Byabato Curry (Reginald) wa Frisco, Texas, William Byabato wa Mikocheni Dar es salaam na Robert Byabato (Delilah) wa Frisco, Texas: Pamoja na Wajukuu Dorothy, Daniel, Kendra, Ingrid, Ethan, Adoree, Jayden, Robert Jr., Isabella na Braxton.
Dada zake Tereza, Leonida na Maria.
Mazishi yatafanyika Bwanjai, Bukoba, ijumaa, June 16. Kutakuwa na misa ya kumuaga marehemu jumatano tarehe 14, saa sita mchana katika kanisa la St Peters, Oysterbay, Dar es salaam.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina la bwana libarikiwe.
Hivyo makala TAARIFA YA MSIBA
yaani makala yote TAARIFA YA MSIBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA YA MSIBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/taarifa-ya-msiba.html
0 Response to "TAARIFA YA MSIBA"
Post a Comment