Loading...
title : TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA
link : TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA
TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA
Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mara ya kwanza kimeanzisha Masomo ya Shahada ya kwanza (Degree) katika fani za Uhazili na Utunzaji wa Kumbukumbu, Taarifa na Nyaraka.
Kufuatia kuanzishwa kwa masomo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Mkuu wa Chuo Dkt. Henry Mambo ametoa wito kwa watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa kuchangamkia nafasi hizo za masomo kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Dkt. Mambo alisema masomo hayo ya Shahada ya kwanza yataanza Mwezi Septemba,2017 katika Matawi ya Dar es Salaam na Tabora, nayo ni hatua kubwa kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika kuwaendeleza Watumishi na Watanzania Kitaaluma.
Kwa upande wa sifa za kujiunga na masomo hayo ya shahada ya kwanza, Dkt. Mambo alisema muombaji anatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha sita pamoja na ufaulu katika masomo mawili au Diploma katika fani husika yenye ufaulu au GPA alama 3.
Mkuu wa Chuo pia aliendelea kufafanua kwamba Masomo hayo ya ngazi ya Shahada yameanzishwa ili kuhakikisha kwamba watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa za kujiunga wanakabiliana na changamoto zinazojitokeza katika soko la ajira kufuatia mabadiliko ya teknolojia na mifumo mbalimbali ya utendaji kazi.“Kutokana na mabadiliko hayo ni vema Watumishi wa Umma na Watanzania wenye sifa kwa ujumla nao wakapata mafunzo ambayo yatawawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la ajira,”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Henry Mambo, katika moja ya hafla jijini Dar es Salaam hivi karibuni(Picha na Maktaba) .
Hivyo makala TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA
yaani makala yote TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/tpsc-yaanzisha-mafunzo-ya-shahada-ya.html
0 Response to "TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA"
Post a Comment