Loading...
title : VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA.
link : VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA.
VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA.
Mwambawahabari
Na Maria Kaira
Mwenyekiti wa wanawake CCM (UWT) wilaya ya Ubungo na Kinondoni Frolence Masunga amewataka viongozi watakaoshindwa kwenye uchaguzi wa nafsi ya matawi ndani ya chama hicho kushirikiana kikamilifu na viongozi watakaopita ili kuleta maendeleo ndani ya chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao maalum cha halmashauri kuu ya wilaya ya ubungo na kinondoni Leo hii bi. Frolence amesema viongozi hao wakiungana kwa pamoja na kuacha makundi makundi wataleta mabadiriko katika chama hicho wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unakaokuja.
"Huu ni uchaguzi mkubwa utakaozingatia haki na sheria,atakaye shindwa naomba akubaliane na matokeo,pia asikate tamaa nafasi zipo nyingi anaweza kugombea nafasi nyingine ya uongozi katika chama na akapata, lengo letu ni kuimarisha chama ili kisonga mbele na sivinginevyo”
“Pia namsihi kiongozi atakayechaguliwa asijibweteke afanye kazi kwa bidii na kuleta maendeleo ya chama " amesema
Mkutano huo umeweza kuhuzuliwa na wanachama wa chama hicho,wajumbe wa halmashaur kuu ya wilaya kutoka kwenye kata na wakuchaguliwa,pia amesema nafasi zitakazo gombaniwa ni pamoja na makatibu matawi,wenyeviti matawi na uenezi matawi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kata ya Ubungo AlhajMarussu Msil amesema uchaguzi huo utazingatia ulinganifu wa kijinsia,ambapo mgombea anatakiwa awe mwanachama halali wa chama hicho na kujikita katika kuleta maendeleo
“Mshindi atakapopatikana tujitahidi kumuunga mkono ili kuleta mabadiriko katika chama na wananchi wetu na sio kununu na kuanzisha vikundi visivyokuwa na maana badala ya kufanya kazi,”amesema
Hivyo makala VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA.
yaani makala yote VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/viongozi-wa-matawi-ndani-ya-ccm.html
0 Response to "VIONGOZI WA MATAWI NDANI YA CCM WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA."
Post a Comment