Loading...
title : WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA
link : WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA
WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA
Mwambawahabari
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameuagiza
Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kupeleka wahandisi wa
kutosha katika ujenzi wa Gati ya Mtwara ili kupata uzoefu katika kazi za ujenzi.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo Waziri
Prof. Mbarawa amesema ushiriki wa wahandisi hao utasaidia kuwajengea uzoefu
mkubwa na hivyo kuokoa fedha nyingi ambazo zitatumika kwa kuwatumia wahandisi wa
kigeni.
“Mradi huu unagharimu fedha nyingi hivyo ni muhimu wahandisi wa TPA wakaja
kujifunza kwa vitendo ili mradi utakapokamilika wahandisi wetu watumike kufanya
ukarabati na matengenezo badala ya kusubiri kuwaleta tena wahandisi kutoka nje”,
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amesisitiza uongozi wa TPA kutafuta wahandisi waliomaliza vyuo nchini ili waweze
kujifunza kwa vitendo kupitia mradi huo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo ili kupata
uzoefu.
Kwa upande wake, Meneja wa bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara, amemhakikishia
Waziri Prof. Mbarawa kuwa tayari utekelezaji wa agizo la kutafuta wahandisi hao
umeshaanza na hatua inayofata ni kuwasili kwa wahandisi hao eneo la madi.
Upanuzi wa bandari ya Mtwara utahusisha awamu nne na awamu ya kwanza ambayo
itagharimu kiasi cha Tsh. bilioni 137 na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 22,
kukamilika kwa gati hiyo kutaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli ya ukubwa wa mita
300 na kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia usafirishaji wa gesi, saruji, korosho pamoja
na makaa mawe.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (kulia), akimuonyesha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, eneo ambalo ujenzi wa
gati ya pili ya bandari hiyo utakapoanza kujengwa wakati Waziri huyo alipokagua vifaa
vya Mkandarasi vilivyowasili katika eneo la mradi hivi karibuni.
Baadhi ya Vifaa ambavyo vitatumika katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara
vikiwa vimeshawekwa site tayari kwa kuanza ujenzi. Ujenzi huo unakadiriwa kukamilika
ndani y amiezi 22.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti
ya Blue), akiangalia vifaa vitakavyotumiwa na Kampuni ya M/S China Railways
Construction Engineering Group (CRCEG) na M/S China Railways Major Bridge
Engineering Group Co. ltd (CRMBEG) katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara,
mkoani humo hivi karibuni.
Hivyo makala WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA
yaani makala yote WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wahandisi-wazawa-kuhusishwa-ujenzi_30.html
0 Response to "WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA"
Post a Comment