Loading...
title : Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji.
link : Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji.
Na.Mwashungi Tahir Maelezo
MAMLAKA Ya Udhibiti wa Huduma za Maji na
Nishati ZURA Imeanzisha Baraza la Watumiaji la Zura ili
kuweza kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na matatizo ya
huduma ikiwemo Maji Umeme na Gesi.
Hayo aliyasema huko kwenye Ofisi ya
Zurailiopo Maisara mwasilishaji
MwanasheriaMwandamizi ZURA Rashid Abdullah
Fadhil alipokuwa akiwasilisha madaya Baraza
laWatumiaji wakati alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari.
Alisema Baraza la Watumiaji la Zura ni Baraza la
Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa ambalo limeanzish
wa chini ya kifungu Nam 33 cha sheria ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Nam
7.2013. Akielezea lengo la kuanzishwa kwa baraza hilo ni
kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa Huduma za Maji
na Nishati Umeme , Mafuta na Gesi kwa kuwa mtumiaji anatumia huduma ya maji na
Nishati mara kwa mara au ameshawahi kutuma moja ya
bidhaa zinazodhibitiwa na ZURA.
Aidha alisema kazi za
BarazalaWatumiaji linatekeleza majukumu yake
kisheria kwa kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa
Hudumazinazidhibitiwa na Zura kwa kufanya maamuzi ,
kutoa maoni na taarifa pamoja nakushauriana na Mamlaka ,
pamoja na Wizara husika.
Pia alisema kazi nyengine ya Baraza hilo ni kupokea
na kusambaza taarifa kuhusu maslahiya watumiaji wa
Huduma zinazodhibitiwa na Zura na pia kushauriana na
wenye viwanda vikubwa , Serikali na vikundi vya watumiaji
vya sekta zinazodhibitiwa.
Akifafanua kuhusu njia za kuwasilisha malalamiko
alisema baada ya kufuata taratibu zote za kuwasilisha
malalamiko mtumiaji atatakiwa kuwasilisha malamamiko
moja kwa moja kwenye kitengo cha huduma kwa Wateja cha
mtoa Huduma wake.
Vile vile alisema endapo malalamiko
yake hayatofanyiwa kazi, mlalamikaji anapaswa kuwasilisha
malalamiko yake ZURA , akipeleka nakala ya barua ya
malalamiko kwa Baraza la Watumiaji kumuwezesha
kufuatilia maendeleo ya shauri usika.
Nae Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhusiano wa Mamlaka
yaUdhibitiwaHuduma ya Maji na Nishati ZURA Khuzaimat
Bakar Kheir aliwatakawananchi walitumie baraza hilo
ili kuweza kutatua migogoroyao kwa kupitia mpango maalum .
Pia alisema elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi
ili waweze kufaidika na baraza hilo ambalo liko kwa ajili
ya kutatua changamoto za wananchi katika utumiaji wa
huduma hizo.
Sheria yaZURA kwa kupitia kifungu cha 33
kkimefafanua uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Watumiaji
linatakiwa liwe na Wajumbe wasiopungua watano (5) na
wasiozidi saba(7) ambao wajumbe hao wanatokana na
Taasisi zisizo za Kiserikali ambazo zinatambulika kisheria
hapaZanzibar ambao watateuliwa na Waziri
anayeshughulikiaZURA.
Mwisho.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO.
Hivyo makala Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji.
yaani makala yote Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/mamlaka-ya-udhibiti-wa-huduma-za-maji.html
0 Response to "Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Aazisha Baraza la Watumiaji."
Post a Comment