Loading...
title : Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji
link : Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji
Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji
Frank Mvungi-Maelezo.
Takriban wakazi 234,398 wa Chalinze watanufaika na mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika Jimbo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa Serikali inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi katika kutekeleza mradi huo.
“Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ndio maana tumeweka wataalamu wetu hapa kumsimamia mkandarasi ili afanye kazi kwa ubora na kwa kasi kama ambavyo Waziri Mkuu aliagiza alipotembelea mradi huu mwezi Machi mwaka huu”, alisisitiza Lwenge.
Akifafanua, Mhandisi Lwenge amesema kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya tatu ni ulazaji wa mabomba ya kusafirisha na ya kusambaza maji, ujenzi wa matanki 19, na ujenzi wa mtambo wa kusafishia maji ambao unaendelea.
Kazi nyingine zinazoendelea katika kutekeleza mradi huo ni ujenzi wa vituo 351 vya kuchotea maji ambapo vituo 27 vimekamilika,vituo 226 vipo katika hatua mbalimbali na vituo 98 havijaanza kujengwa.
Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Lwenge amesema kuwa ni kuongezeka kwa upatikanaji wa vifaa kwa wakati katika eneo la mradi, kuongeza wafanyakazi na maeneo ya kazi na kuteua mwakilishi wa kampuni anayeweza kutoa maamuzi kwa niaba ya kampuni inayotekeleza mradi.
Aidha, Waziri Lwenge amesema kuwa Serikali itatoa ufumbuzi wa changamoto ya wananchi wa Jimbo hilo kulipia malipo ya huduma (service charge) hata pale wanapokuwa hawajapata huduma hiyo ili kuwe na utaratibu mzuri unaowezesha wananchi kulipia huduma pale wanapotumia tu na si vinginevyo.
Moja ya tenki la maji linalojengwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu ikiwa ni sehemu ya mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la ChalinzeChalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete akimshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
Mafundi wakiendelea na maandalizi ya ujenzi wa matenki yakuhifadhi maji katika chanzo cha maji Ruvu. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji
yaani makala yote Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wakazi-234398-wa-chalinze-kunufaika-na_5.html
0 Response to "Wakazi 234,398 wa Chalinze kunufaika na mradi wa maji"
Post a Comment