Loading...

Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji

Loading...
Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji
link : Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji

soma pia


Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji

Wakazi wa Kijiji cha Ngulu kitongochi cha Mkongea wilaya ya Mwanga wamesema kuwa tatizo la maji limekuwa tatizo sugu kwa muda mrefu bila kutatuliwa hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika. Mkazi wa kijiji hicho, Halima Miraji alisema kuwa tangu mwaka 2004 wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo kwa muda mrefu sasa maji yamekuwa yakitoka usiku wa manane tu.

Halima alisema kuwa mfumo wa maji ulijengwa kwenye kijiji jirani cha Mgagani mwaka 1992 ambapo vijiji vyote viwili vilikuwa vikipata maji kutokea hapo. Hata hivyo, alisema wakati wa mafuriko, miundombinu iliharibika na hivyo kusababisha maji yapungue na ndipo viongozi wa vijiji hivyo viwili walipoamua kuwa maji yawe yanafunguliwa kwenye kijiji cha Ngulu nyakati ya mchana na kijiji cha Ngulu wakati wa usiku.

“Kutokana na changamoto hiyo, wanawake tunalazimika kuamka usiku wa manane kuchota maji kwa kuwa kwa kawaida huwa yanakatika alfajiri,” alisema Halima. Alisema kwa kuwa wanawake ndio wanaochota maji usiku na badhi ya wanaume wachache ambao hawajaoa, kutokana na hilo alisema kuwa badhi ya wanawake walijikuta wakiianza uhusiano na wanaume jambo ambalo limefanya ndoa zao kuvunjika.

Alisema kila mtu hulazimika kuweka ndo moja kwenye foleni ya maji iliyo na watu Zaidi ya hamsini kabla ya mzunguko kurudia mara ya pili, tatu na kadhalika jambo ambalo liliwafanya badhi ya wanawake kuingia kwenye vishawishi wakati wanasubiri kwenye foleni. Alisema kuwa changamoto nyingine, ni kuwa shughuli nyingi kama kilimo, biashara na kutunza familia zimekuwa zikizorota kwa kuwa wanakuwa wamechoka asubuhi baada ya kuchota bmaji usiku kucha.
Mkuu wa Wilaya yaMwanga, mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho.





Hivyo makala Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji

yaani makala yote Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wakazi-wa-kijiji-cha-ngulu-walia-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wakazi wa Kijiji cha Ngulu walia na tatizo la maji"

Post a Comment

Loading...