Loading...
title : WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI
link : WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI
WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI
Mwambawahabari
Na Tiganya Vincent
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kwa ngazi zote kuanza kuwasaka watu wanaopita pita katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwatapeli wananchi kuwa wanaweza kuwapatia fursa za Kujiunga na Jeshi la Taifa kinyume cha utaratibu uliowekwa na Jeshi hilo.
Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo juzi Wilayani Tabora wakati akifunga mafunzo wa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Opereshi Magufuli katika Kikosi cha Jeshi cha 823 Msange JKT .
Mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa ni vema sasa Kamati hizo kutoka chini hadi juu kuangalia kwa ukaribu taratibu zinazotumika katika kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili kuwabaini matapeli ambao wamekuwa wakiwalaghai wananchi na kuwatoza pesa ili wawasaidie kujiunga na Jeshi hilo, jambo ambalo ni uongo.
Awali Mkuu wa Bregedi ya 202 kundi la Vikosi vya Kanda ya Magharibi (FARU) Brigedia Jenerali Stephen Mkumbo alisema kuna haja ya viongozi wa Mkoa kushirikiana katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya taratibu za kujiunga na JKT ili kuwasaidia wasije au wasiendelee kutapeliwa fedha zao.
Alisema kuwa Makao Makuu ya JKT wakitaka vijana wa kujiunga na Jeshi hilo wanaandika barua ya kuomba vijana na kujiunga na JKT ikiwa na masharti yanayotakiwa na kuipeleka kwenye Mikoa yote ambayo nao uandika barua ya aina ile ile na kuipeleka Wilayani nao wanashusha hadi ngazi za vijiji na sio vinginevyo.
Brigedia Jenerali huyo aliongeza kuwa mchujo uanzia ngazi za Kata na ndipo unaingia ngazi ya Wilaya na mwisho Mkoa ambapo Maafisa wa JKT uungana nao katika kuwasaili vijana na ndipo upata wanaostahili kujiunga na Mafunzo ya Awali katika Kambi zao mbalimbali.
Alisema kuwa matapeli hao wamekuwa wakiwaibia wananchi kwa kuwatoza kuanzia shilingi laki 5 hadi milioni moja kwa madai kuwa watawasaidia kupata fursa za kujiunga na JKT jambo ambalo ni uongo na sio utaratibu unaotakiwa.
Brigedia Jenerali Mkumbo aliwaomba viongozi wa Mkoa wa Tabora kusaidia kutoa elimu juu ya utaratibu wa kujiunga na JKT ili wananchi wasaidie kuwafichua matapeli hao kwa ajili kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria .
Akisoma risala ya wahitimu wenzake 870 wa mafunzo ya awali Fred Mashauri alitoa wito wa kuongezwa kwa idadi ya vijana wa kujitolewa ikiwemo walemavu ili nao wapate fursa za kupata mafunzo ya uzalishaji mali na stadi za maisha .
Hivyo makala WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI
yaani makala yote WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/wanaotapeli-wananchi-kuhusu-nafasi-ya_12.html
0 Response to "WANAOTAPELI WANANCHI KUHUSU NAFASI YA KUJIUNGA NA JESHI WASAKWE HARAKA -MWANRI"
Post a Comment