Loading...

ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu

Loading...
ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu
link : ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu

soma pia


ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar Dkt. Said Seif Mzee (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mliasili, Mifugo na Uvuvi Dkt. Juma Ali Shehena ya vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kuimarisha vitalu vya miche ya mikarafuu.
Picha na Ramadhani Ali.

Na Ramadhani Ali – Maelezo  

Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) limeikabidhi Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi  vifaa kwa ajili ya kuendeleza vitalu vya miche ya mikarafuu vyenye thamani ya shilingi milioni 26 na fedha taslimu milioni kumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZSTC Dkt. Said Seif Mzee amemkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dkt. Juma Ali kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo katika hafla iliyofanyika Wizarani Maruhubi.

Dkt Said amesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakishirikiana na Idara ya Misitu na Mali zisizorejesheka katika mambo yanayoongeza tija katika uzalishaji wa miche ya mikarafuu na pia katika kutoa elimu kwa wakulima wa karafuu juu ya njia bora ya kupanda kuhuisha na kuzichuma.
Mkurugenzi Mtendaji alieleza kuwa Shirika katika kuendeleza zao la karafuu litaendelea kutoa misaada ya kuimarisha taasisi za Serikali na taasisi za watu binafsi zenye nia ya kuimarisha zao hilo kubwa la kiuchumi Zanzibar.

Amekumbusha kwamba katika mwaka 2015/2016 Shirika Shirika lilitoa msaada wa wenye thamani ya shilingi milioni 70.8 kwa Idara  ya Misitu na kuvisaidia vikundi 10 vinavyootesha miche ya mikarafuu yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki nne.

Akipokea vifaa hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo alisema Wizara itaendeleza juhudi za Serikali ya kuhakikisha inazalisha zaidi ya  miche milioni  moja kwa mwaka Unguja na Pemba katika kuhakikisha zao hilo linaendelea kuimarika.
Amesema watahakikishia wanafuatilia miche mipya iliyopandwa mwaka huu ili kuona inakua vizuri na hatimae kutoa mavuno makubwa miaka michache ijayo.

Vifaa vilivyokabidhi  ni pamoja na nyavu za vitalu za kivuli na paipu za kujengea vitalu, saruji, kamba, nondo, mchanga, kokoto kwa ajili ya kuchimba visima vipya vya kumwagilia maji vitalu.


Hivyo makala ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu

yaani makala yote ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/zstc-yakabidhi-vifaa-vya-kuendeleza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZSTC yakabidhi vifaa vya kuendeleza vitalu vya miche ya karafuu"

Post a Comment

Loading...