Loading...
title : ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO!
link : ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO!
ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO!
Na Ankal
Hebu jaribu kulielezea jiji la Dar, au la Arusha, ama la Mwanza, Mbeya ama jiji lolote lile, tena kwa kutumia ukurasa mmoja tu na uwe umefanikiwa kulieleza kinagaubaga kiasi hata mtu ambaye hajawahi kufika hapo ajione kama keshafika na anapafahamu vizuri.
Basi huo ndio mtihani nilionao wakati naandika haya, tena kwa moyo mzito, nikijaribu kumwelezea rafiki yetu, kaka yetu, ndugu yetu, jamaa yetu au vyovyote vile upendavyo kumwita mtu kama Balozi Abdul Omar Cisco Mtiro.
Labda uamue uzungumzie kamtaa kamoja tu katika kitongoji kimoja, ndio kidooooogo unaweza kufanikiwa kueleza vitu vikaeleweka...Nami ndivyo naitajaribu kufanya hapa, kwa kudonyoa kasehemu kamoja tu ka Braza Cisco.
Ni kweli kwamba mtu akitangulia mbele ya haki huwa kuna hulka ya kumsifia na kumuenzi mtu huyo. Lakini si uwongo kwamba haya niandikayo hapa, japo yalikuwa nyuma ya ubongo wa wengi wetu siku zote, ni halisi na wala sio kwa sababu Cisco hatunaye tena.
Kwa wengi alikuwa mkarimu na mwingi wa bashasha saa zote.
Kwa tuliobahatika kuwa karibu naye, Cisco alikuwa hivyo na zaidi. Pamoja na kuwa na wadhifa mkubwa serikalini (Balozi wetu nchini Nigeria na Malaysia katika nyakati mbalimbali na baadaye Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje), Cisco alikuwa mtu wa kujichanganya na kila mtu bila kujali hali ama mali zake. Hakuwa na makuu wala makidai.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Hivyo makala ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO!
yaani makala yote ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO! Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO! mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/adios-amigo-braza-cisco.html
0 Response to "ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO!"
Post a Comment