Loading...
title : Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo
link : Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo
Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo
Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeondoka alfajiri ya leo, tayari kabisa kucheza na mabingwa wa ligi kuu nchini Rwanda timu ya Rayon Sports mchezo wa kirafiki kwa timu hiyo kusheherekea Ubingwa wao siku ya Jumamosi
Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo kwenye maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara na mara baada ya mchezo huo, kikosi hicho kitaanza safari ya kurejea nchini Jumapili ijayo.
Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi na Ngao ya Jamii msimu uliopita, wanaendelea na mazoezi huku ikiwakosa wachezaji wake kadhaa akiwemo nahodha msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, beki Erasto Nyoni, kiungo Salmin Hoza na washambuliaji Mbaraka Yusuph na Shaaban Idd, ambao wako na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Nyota hao wako na Stars inayoshiriki michuano ya Kombe la COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini, ambapo hii leo Stars itajitupa uwanjani kuvaana na Zambia katika mchezo wa hatua ya Nusu Fainali.
Wengine ambao bado hawajawasili ndani ya kikosi cha Azam ni mabeki Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, Eneock Atta Agyei (Ghana), kiungo Mcameroon Stephan Kingue na mshambuliaji Wazir Junior, aliyesajiliwa akitokea Toto Africans ya Mwanza.
Hivyo makala Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo
yaani makala yote Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/azam-fc-yawafuata-mabingwa-wa-ligi-kuu.html
0 Response to "Azam FC yawafuata mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda alfajiri ya leo"
Post a Comment