Loading...

Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri

Loading...
Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri
link : Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri

soma pia


Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri

Benki ya KCB Tanzania inaendelea kuwapatia wanawake wajasiriamali waliopitia mafunzo ya ujasiriamali ya KCB 2jiajiri ushauri wa kibiashara kwa vitendo ofisini kwa wafaidika wa 2jiajiri. 

Maafisa watatu ambao ni; afisa fedha, sheria na masoko wanawatembelea wafaidika hao wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya KCB 2jiajiri katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.

KCB 2jiajiri ni programu inayolenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kukua na kuwa endelevu. Matatizo yanayolengwa kutatuliwa kutoka kwa wanawake wajasiriamali hawa ni elimu ya kifedha, kufikiwa na huduma za kifedha, ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji, utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa n.k.

“Programu hii ilizinduliwa rasmi Desemba, 2016, ambapo hadi sasa tumewapa stadi za biashara endelevu wanawake wajasiriamlai 258 kutoka mikoa 6 ya Tanzania.” Alisema Christine Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB.

Akielezea kuhusiana na programu ya KCB 2jiajiri Bi. Manyenye alieleza kuwa, wafaidika wa KCB 2jiajiri baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu darasani, kwa sasa wananufaika kwa kupata ushauri wa kibiashara na kitaalamu kutoka kwa washauri watatu katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko.
Afisa Sheria Bi. Doris Mugarula (wakwaza kushoto) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimsikiliza mjasiriamali Bi. Batula akielezea maendeleo ya biashara yake ya nguo mkoani Arusha. 
Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (wakwanza kulia) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kulia) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Shamsa Ally (kushoto) katika duka lake la vifaa vya magari makubwa mkoani Morogoro.
Afisa Masoko, wa Benki ya KCB, Bi. Ghati Muhere (kulia), akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Jac Bazaar (kushoto) katika duka lake la vifaa vya umeme mkoani Morogoro.
Afisa Masoko Bi. Ghati Muhere (aliyechuchumaa) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (aliyesimama) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Violeth (aliyeinama) katika biashara yake ya kilimo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Masoko, Bi. Ghati Muhere (wakwanza kulia), Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (watatu kushoto) na Afisa Fedha, Bi Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Mercy (wakwanza kushoto) katika biashara yake ya huduma za Interneti mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.



Hivyo makala Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri

yaani makala yote Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/benki-ya-kcb-tanzania-yaendelea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri"

Post a Comment

Loading...