Loading...
title : DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR
link : DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR
DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameshiriki katika mazishi ya watoto wanne waliofariki dunia jana (juzi) baada ya kuingia kwenye gari iliyokuwa sehemu ya maegesho na likajifunga hali iliyopelekea watoto hao kukosa hewa na kufariki huko Kidongo Chekundu Unguja.
Marehemu hao waliotambuliwa kwa majina ya Mwatma Mohamed Malawi (2), Haisam Mustafa(2), Munawar Ahmed Khamis (3) na Muslim Hamza bakar (2) wote wamezikwa leo katika maeneo tofauti ya Makaburi ya Mwanakwere na Kiembe samaki Mbuyu Mnene Unguja.
Akizungumza mara baada ya maziko hayo Naibu Katibu huyo huko katika makaburi ya Mwanakwerekwe, alisema CCM imepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa ya vifo vya watoto hao na inatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizopata msiba huo na kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba huo.
Alisema watoto hao walitarajiwa kuwa ni miongoni mwa viongozi na wataalamu wa fani mbali mbali wa baadae hivyo msiba huo umeacha pengo kubwa kwa familia na taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt. Mabodi aliwataka wazazi na walezi nchini kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha mazingira yanayotumiwa na watoto kucheza yanakuwa katika hali ya usalama ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha majeraha ama vifo kwa watoto wao.
Maiti za watoto wanne waliofariki ndani ya gari huko Kidongochekundu Zanzibar wakitolewa msikitini na kupelekwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya mazishi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao.
Hivyo makala DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR
yaani makala yote DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/dktmabodi-ashiriki-mazishi-ya-watoto.html
0 Response to "DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR"
Post a Comment