Loading...
title : Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone
link : Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone
Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone
Na:Said Salim “Hazard” kutoka Mbulu, Manyara.
Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Kombain ya Mjini Unguja imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya wapinzani wao Saint Patrick Academy ya Arusha kushindwa kusafiri kwenda Mbulu Mkoani Manyara wakitokea huko Arusha kucheza na wapinzani wao Mjini mchezo ambao wa nusu fainali ulikuwa usukumwe kesho majira ya saa 10 za jioni katika uwanja wa Julius Nyerere.
Akithibitisha taarifa hizo Mwenyekiti wa Mashindano hayo Wilium Zongwe (Dell Piero) amesema Saint Patrick Academy wameshindwa kwenda huko Mbulu kutokana na gharama za fedha hivyo Mjini Unguja wametinga wao moja kwa moja fainali.
“Saint Patrick Academy washatoa taarifa kama hawatoweza kufika Mbulu kesho katika mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Mjini kutokana na uhaba wa fedha, hivyo Mjini wameshafanikiwa kufika fainali moja kwa moja”.
Lakini inasemekana kuwa timu ya Saint Patrick Academy ya Arusha imewaogopa Mjini Unguja baada ya kutoa dozi nene hasa baada ya jana kuwachapa Lindi academy kwa mabao 5-1 huku magoli ya Mjini yalifungwa na Ibrahim Abdalla (Imu Mkoko ) 2, Mohamed Mussa (Modi) 2 na Mohamed Haji (X Box) 1, hivyo sababu ya kushindwa kumudu gharama ni kisingizio tu.
Kwa maamuzi hayo Mjini Unguja watasubiri kucheza fainali siku ya Jumanne ya July 18, 2017 na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya JKU Academy kutoka Zanzibar au Fire Boys kutoka Karatu Arusha.
Hivyo makala Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone
yaani makala yote Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/kombaini-wilaya-ya-mjini-yatinga.html
0 Response to "Kombaini Wilaya ya mjini yatinga Fainali mashindano ya Rolling Stone"
Post a Comment