Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL
link : MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Dk. Jane Goodall, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika Ujumbe wake Dk. Goodall aliambata na Mama Getrude Mongela na Hadija Simba ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Roots and Shoots pamoja na watendaji wengine wa Taasisi hiyo.
Katika mazungumzo yao Dk. Goodall pamoja na mambo mengine amezungumzia uharibifu wa shoroba za wanyama pamoja na makazi yao katika hifadhi ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma ambayo ni maarifu kwa uhifadhi wa Sokwe. Alisema kwa sasa hifadhi hiyo imezungukwa na maakazi ya binadamu hali iliyosababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wanyama hao.
Aidha Dk. Goodall alimuelezea Makamu wa Rais jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kupambana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya Gombe ikiwemo kuhimiza uwepo wa mipango bora ya matumizi ya ardhi.
“inawezekana tatizo kubwa linalosababisha uharibu wa mazingira ni umasikini na uelewa mdogo wa wananchi” alieleza Dk.Goodall. Hata hivyo alisema zipo jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kutoa elimu kwa umma. Kwa sasa wananchi kutoka katika vijiji zaidi 52 mkoani wa Kigoma wanapatiwa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Vilevile, jumla ya shilingi Milioni 400 zimekopeshwa kwa wananchi wa vijiji 32 ili kujiwezesha kiuchumi na kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan yenye leno la kulinda shoroba na makazi ya Sokwe. Hali hii imeanza kuleta mafanikio.
Dk. Goodall ametaja changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ya Gombe kuwa ni kuwepo kwa wakimbizi kutoka Burundi ambao kwa kiasi kikubwa hushiriki katika shughuli ambazo husababisha uharibu wa mazingira kama vile kilimo na ufugaji usio endelevu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na akiwa kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe kutoka kwa Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-akutana-na-jane-goodall.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA JANE GOODALL"
Post a Comment