Loading...
title : Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania
link : Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania
Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo ni kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia ambayo imelenga kushughulikia masuala uwezeshwaji wa wanawake na huduma za afya akisema kwamba wamekuja nchini kwa wakati mwafaka,
Wakati wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation Makamu wa Rais alisema kuwa Merck Foundation inakaribishwa na serikali inatarajia kushirikiana na taasisi hiyo inayoheshimika na iliyo makani katika kuwezesha wanwake , vijana, huduma za afya na sayansi.
Tunatambua mchango unaotolewa na Merck Foundation katika kujengea uwezo huduma za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli zake nchini Tanzania, hususani katika kampeni zinazolenga kuuongezea umma uelewa kuhusu ugumba.
Makamu wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini Tanzania na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni mpya katika kuheshimu na kumtambua wanawake kama sehemu ya wanajamii wanaozalisha wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.”
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Ofisa Mkuu Mtendaji wa Merck Foundation, Dk Rasha Kelej, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mkuu Mtendaji wa Merck Foundation, Dk Rasha Kelej, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.
Hivyo makala Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania
yaani makala yote Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-apongeza-juhudi-za-merck.html
0 Response to "Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania"
Post a Comment