Loading...

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM

Loading...
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM
link : MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM

soma pia


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM

Mwambawahabari


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua Taarifa ya Nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).

Uzinduzi huo  ulihudhuriwa na  kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo  la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Sylvia Mabandla, Viongozi wengine wa APRM Tanzania ni Balozi Ombeni Sefue, Profesa Hasa Mlawa na Balozi Aziz Mlima aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

APRM ni mpango wa hiari wa kujipima kwa vigezo vya utawala bora uliobuniwa mwaka 2003 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Lengo la mpango huu ni kuziwezesha nchi  wanachama kujitathmini kwa vigezo vya utawala bora katika maeneo manne ambayo ni; Demokrasia na Utawala wa Kisiasa; Usimamizi wa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya Biashara; na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.

Akihutubia katika uzinduzi huo, Makamu Rais amewapongeza Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki katika mchakato wa APRM kwa ujasiri wao wa kushirikishana taarifa za kuaminika kuhusu masuala ya utawala bora katika nchi zao.

 “Taarifa hizi zinaonesha wazi juu ya hali ya utawala bora katika Bara letu na kutupa nafasi ya kujirekebisha pale ambapo kuna dosari na kujipongeza pale tunapofanya vizuri na kuwapa wengine nafasi ya kujifunza zaidi’’ alisema Makamu wa Rais.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha kitabu chenye ripoti  ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



Baadhi ya wageni mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Mkutano huo.


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-mhe-samia-azindua-ripoti_19.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM"

Post a Comment

Loading...