Loading...

MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE

Loading...
MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE
link : MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE

soma pia


MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE

MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewapongeza wanawake wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Ametoa pongezi hizo leo (Jumamosi, Julai 22, 2017) wakati akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Ileje katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi.Ametoa pongezi hizo baada ya kushiriki katika ukaguzi wa vikundi mbalimbali vya wanawake wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali wilayani Ileje.

Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe, amesema ujasiriamali ni mkombozi kwa wanawake.

Mama Mary amesema amefarijika kuona wanawake wengi wakishiriki katika shughuli za ujasiriamali kwa kuwa zinalenga kuwaongezea kipato na kuwakwamua kiuchumi.Mmoja wa wajasiriamali hao, Bi. Riziki Sunday amesema shughuli hizo za ujasiriamali zimemuwezesha kumudu mahitaji ya familia yake, hivyo kuondokana na utegemezi.

Bi. Riziki amesema kuwa miongoni mwa faida alizozipata kutokana na ujasiriamali ni pamoja na kujenga nyumba, kusomesha watoto na kuongeza mashamba.

Pia Bi. Riziki ametumia fursa hiyo kuwashauri wanawake wenzake kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakitazama vifaranga wa samaki wakati alipotembelea banda la Kikundi cha wanawake cha Tukazane cha Ileje kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Hivyo makala MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE

yaani makala yote MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/mke-wa-waziri-mkuu-apongeza-wanawake.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE"

Post a Comment

Loading...